Thursday, August 20, 2009

Ningekuwa Spika Sitta Ningejiuzulu!


NINGEKUWA SPIKA SITTA NINGEJIUZULU

HAKI ya Mungu kweli duniani kuna mambo pamoja na mambo yote mazuri ambayo spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samuel Sitta kwa Wabunge wa chama cha mapinduzi wakiwemo na Mafisadi ambao wanajulikana kwa majina mimi sitaki kuwataja bado wabunge hao ambao wengine ni wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (NEC) na mafisadi wamo wamememgeuka!

Jamani kwa kweli ni lazima tukajifunza ustaarabu mengi sita kawasaidia wabunge hawa pamoja na wale wa upinzani lakini sasa tena moto umemgeukia yeye jamani kweli hii ni fair?
Hapa naorodhesha tu mambo machache ambayo spika sitta amewapigania wabunge hawa na kubalansi Bunge ili liliemee upande mmoja halafu akaonekana kana kwamba anapendelea upande mmoja wa CCM!

Spika huyuhuyu ambaye anaitwa Mbabe amepigania kwa nguvu marupurupu ya wabunge na kusababisha sasa hivi wabunge kulipwa mshahara tu kiasi cha sh. Milioni 12 kwa mwezi na marupurupu kibao!

Hiyo haikutosha spika huyohuyo mbabe amepigania mpaka sheria ya kuanzishwa mfuko wa maendeleo ya Jimbo kwa wabunge umepita kwa mbinde Bungeni licha ya wananchi kuonyesha kuukataa!

Mimi sijatumwa na Mtu kuzungumzia hili suala ila nimeguswa na kitendo alichofanyiwa hivi karibuni Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Nec wa kutaka avuliwe uanachama kwa kuwa anaendesha eti Bunge kibabe!

Kwa kweli CCM hamkumfanyia Spika wenu sawa kabisa kwa sababu mnataka aliendesheje Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hivi sasa limekuwa kama Kikundi cha vichekesho cha orijino Komedi kuna jambo lingine zaidi ya hili si mseme?

Alichokisema hivi karibuni Bungeni spika kuwa anaomba ulinzi wa ziada kwa kuwa nguvu ya mafisadi inamzidi alikuwa sahihi kwa kuwa tayati alishaona nini kinafuata na kwa kuwa serikali haikumuelewa ndiyo maana ilipuuzia na maneno meengi ya kejeli yakatolewa juu ya kauli yake!

Lakini ukweli wa maneno ya Mzee Sitta sasa yamejidhihirisha ndani ya mkutano wa CCM ambamo kunaonekana kuwa CCM bila mafisadi haiwezekani kuwa hai, sasa mnataka spika aendesheje Bunge lenu JAMANI?

Mnataka spika atoe uhai wake ndiyo mbaini kuwa alikuwa anaendesha bunge kwa usawa na kubalansi pia au mnatakaje au aendeshe Bunge kwa kupendelea wabunge wa CCM? Mtalishusha hadhi na viwango pia kama mnataka liwe ambavyo ninyi mnataka liwe!
Kwa hali hii mimi ningekuwa Spika Sitta ningejiuzulu Uspika ili kuwaachia nafasi mafisadi kumtafuta spika ambaye wao wanamtaka ambaye hatendesha Bunge kibabe au sio na kupendelea CCM maana viwango ulivyoahidi mwaka ule havitakuwepo tena!

Kwa kweli inauma halafu inakera zaidi inatia kichefuchefu kufanya hivyo ni kuonyesha ni kiasi gani kwamba CCM inashikiliwa na kuendeshwa na watu wachache wenye pesa zao na utartibu huu ambao CCM mmeuonyesha sijui nini kitafuata lakini mmetia DOA tena doa lenyewe jekundu kwenye nguo nyeupe!

SHAURI YENU CCM angalieni msije mkajuta kwa kuwasafisha watu ambao tayari walishachafuka siku nyingi kupitia watu ambao wangekusaidieni kuwasafisha angalau kwa kutumia busara zao ambazo zinaonekana ni ubabe!