MLEMAVU wa ngozi Mariamu Obedi (18)mkazi wa eneo la Nkhungu mjini Dodoma ameiomba Serikali pamoja na wanachi wamsaidie fedha kwaajili ya matibabu ya kansa ya jicho ili aweze kwenda hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar-es-Salaam kutibiwa.
Ombi hilo alilitoa jana wakati alipokuwa akizungumza na mmiliki wa blog hii mjini Dodoma huku akilia kutokana na maumivu makali anayoyapata yanayosababishwa na uvimbe uliopo katika jicho lake la kushoto kuuma.
Alikielezea kuanza kuugua jicho hilo alisema kuwa kilitokea kiupele kidogo katika jicho hilo na hivyo kuanza kuvimba ikiwa ni pamoja na kumsababishia maumivu makali.
Mariamu alisema kuwa baada yakuona hali hiyo ikizidi kuendelea aliamua kwenda katika hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma kwaajili yakupata matibabu.
Mlemavu huyo wa ngozi (albino) alifafanua kuwa alianza kuumwa mwaka 2007 ambapo alipoenda katika hospitali hiyo ya mkoa wa Dodoma uongozi wa hospitali hiyo ulimwandikia barua aende hospitali ya Mvumi.
Alisema kuwa baada ya kwenda katika hospitali hiyo ya Mvumi pia walishindwa kumtibia na hivyo kumuandikia barua wakimtaka aende jijini Dar-es-Salaam katika hospitali ya Msasani ambapo alikwenda na kufanyiwa oparesheni na kupata nafuu.
Alibainisha kuwa baada ya kupata naafuu alirejea tena Dodoma anapoishi ambapo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo ni 2008 na ilipofika mwaka huu hali hiyo ilimrudia tena na hivyo kulazimika kurudi tena katika hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.
Mariamu anafafanua kuwa alipofika katika hospitali hiyo alipimwa na hivyo kuonekana kuwa ana ugonjwa wa kansa ambapo anatakiwa kwenda hospitali ya Ocean road kutibiwa.
Hata hivyo ameiomba Serikali na watu wenye mapenzi mema ambao wataguswa na tatizo alinilonalo, kumsaidia chakula kutokana na mama yake mzazi Cahrerine Peter kutokuwa na uwezo hali ambayo inamsababisha kulala njaa licha ya yeye kunywa dawa kali na hivyo kumfanya kukosa nguvu kutokana na kukosa chakula.
KAMA UMEGUSWA KUMSAIDIA BINTI HUYU, TAFADHALI WASILIANA KUPITIA NAMBA HII' +255713358273, AU tumia akaunti hii 029201039794, NBC Bank Mazengo Branch.
Mungu akubariki sana.