Monday, October 06, 2014

Hivi ndivyo wagogo wanavyowazika waliokufa kwa kifafa!!!HAYA ndiyo mambo mbayo huyafahamu kuhusu wagogo.
Ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona… ya firauni, mila na desturi za kabila la wagogo bwana kwa mtu ambaye amefariki kutokana na ugonjwa wa kifafa, inakuwaga hivi;
Kwanza akishafariki,ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hawaruhusiwi kuwa karibu na mwili wa marehemu.
Pili akishawekwa katika jeneza hatakikiwi kuagwa kwa imani kwamba mtu huyo ni kama najisi Fulani hivi.
Hii siyo hadithi jamani mimi mwenyewe ni shuhuda wa tukio hili baada ya mjomba wangu kufariki kutokana na ugonjwa huo ambao kwa kigogo unaitwa “UTAMWA WA CHINZILISA”. Haya ninayoyaandika hapa ndiyo yaliyotokea katika msiba huo.
Nilishangaa lakini sikuwa na namna maana ndivyo ndugu zangu wanavyoamini hivyo na  hakuna wa kuwabadilisha mpaka siku wafe na wenyewe.
Baada ya hapo wakishachimba kaburi, mtu huyo hawekwi katika sanduku ua jeneza kama ilivyo ada kwa dini ya kikristo, na badala yake marehemu huwekwa katika ngozi na kuzikwa.
Lakini pia sio huzikwa kama marehemu wengine, huyu alifariki kwa ugonjwa kifafa huzikwa na kila kitu chake, kama vile nguo zake zote, na ninavyoona kama ingewezekana hata nyumba na vitanda vyake navyo pia anatakiwa azikwe nanvyo sema ndo haiwezekani tu, LOH!
Baada ya kuzika, hakuna matanga, kinachotakiwa ni watu kutawanyika na kuendelea na shughuli zao na si vingine.
Ama kweli ukistaajabu ya musa, utayaona ya kigogo, huu nao si unyanyapaa jamani, ndugu zangu wagogo hebu tubadilike jamani maana haya mnayofanya kwa madai kuwa eti ni mila yalishapitwa na wakati na wala hayampendezi Mungu.
Ends………….