Monday, October 06, 2014

Hivi ndivyo wagogo wanavyowazika waliokufa kwa kifafa!!!



HAYA ndiyo mambo mbayo huyafahamu kuhusu wagogo.
Ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona… ya firauni, mila na desturi za kabila la wagogo bwana kwa mtu ambaye amefariki kutokana na ugonjwa wa kifafa, inakuwaga hivi;
Kwanza akishafariki,ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hawaruhusiwi kuwa karibu na mwili wa marehemu.
Pili akishawekwa katika jeneza hatakikiwi kuagwa kwa imani kwamba mtu huyo ni kama najisi Fulani hivi.
Hii siyo hadithi jamani mimi mwenyewe ni shuhuda wa tukio hili baada ya mjomba wangu kufariki kutokana na ugonjwa huo ambao kwa kigogo unaitwa “UTAMWA WA CHINZILISA”. Haya ninayoyaandika hapa ndiyo yaliyotokea katika msiba huo.
Nilishangaa lakini sikuwa na namna maana ndivyo ndugu zangu wanavyoamini hivyo na  hakuna wa kuwabadilisha mpaka siku wafe na wenyewe.
Baada ya hapo wakishachimba kaburi, mtu huyo hawekwi katika sanduku ua jeneza kama ilivyo ada kwa dini ya kikristo, na badala yake marehemu huwekwa katika ngozi na kuzikwa.
Lakini pia sio huzikwa kama marehemu wengine, huyu alifariki kwa ugonjwa kifafa huzikwa na kila kitu chake, kama vile nguo zake zote, na ninavyoona kama ingewezekana hata nyumba na vitanda vyake navyo pia anatakiwa azikwe nanvyo sema ndo haiwezekani tu, LOH!
Baada ya kuzika, hakuna matanga, kinachotakiwa ni watu kutawanyika na kuendelea na shughuli zao na si vingine.
Ama kweli ukistaajabu ya musa, utayaona ya kigogo, huu nao si unyanyapaa jamani, ndugu zangu wagogo hebu tubadilike jamani maana haya mnayofanya kwa madai kuwa eti ni mila yalishapitwa na wakati na wala hayampendezi Mungu.
Ends………….

Wednesday, August 31, 2011

EID MUBARAK!

EID MUBARAK kwa waislam wote duniani

habari njema kwa wenye vitambi na mafuta mengi mwilini

kwa wale ambao wanajijua kuwa wana vitambi, unene uliokithiri, mafuta mengi mwilini, ninayo habari njema kwao, dawa ya kutoa mafuta inapatikana kwa gharama nafuu ya sh. 20000/= elfu ishirini tu, kama unahitaji just call 0713358273, dawa hii inaendana pamoja na kufanya mazoezi kidogo na kupunguza kula vyakula ambavyo vyenye mafuta, mafuta yaisha kabisa na kitambi kinamalizika kabisa wahi sasa.

Wednesday, March 30, 2011

HiLi nI WaZo La LEo


Hawa Jamaa wako Siriaz eti na wanakwambia hivi!!!CHEZEA MSHAHARA, USICHEZEE KAZI!!!!!

Monday, August 02, 2010

Wednesday, June 23, 2010

Et ni kweli kwamba kumkeketa Mtoto wa Kike kunamfanya asiwe Malaya?

HIVI ni Kweli eti kumkeketa mtoto wa kike ni kumfanya asiwe Malaya jamani? Ninauliza hivi nina maana, moja ya mila na tamaduni za wagogo hapo zamani ilikuwa ni kumkeketa motto wa kike ili kumfanya asiwe Malaya.

UNAOBA bwana, unajua kwa nini? Eti wabibi wale wa zamani wanasema kuwa ukimekeketa mtoto wa kike unampunguzia hamu ya kufanya mapenzi na hivyo anakuwa si Malaya!
Sasa sina uhakika kama ni kweli sana, naomba wadau mnisaidie katika hili tafadhali naombeni jamani, naomba mtoe maoni yenu halafu baadaye nitafunga mjadala kwa kuwa bado natafuta materials zaidi ya kuwafahamisha kuhusu mila hii ya mgogo!

Karibuni sana.

Friday, March 05, 2010

HIZI NI SALAMAU ZA WAGOGO KUTOKA KWA KAKA FREDIRICK MUMBULI!

Da Martha,

Nimefurahi kuona kazi nzuri unayoifanaya, ni Tuvuti nzuri ikieendelezwa na ikapata habari nyingi moto moto.

Kumekuwa na jitihada nyingi kukujaribu kuwakumbusha na kuwahamasisha Wagogo kuungana na kufanya kazi za maendeleo na hususani za kiuchumi (Ujasiriamali) lakini nyingi ziko kwa mwendo wa kinyonga, Wanyausi wamebaki na kilio cha Ukame (Chibahu) na umasikini!

Leo hii ukijitambulkisha mgogo haraka kwenye mawazo ya “wanyamunthu” kunakuja wazo la omba omba/masikini, siku hizi tumewafunika hata watani zetu, maana sisi tuna hata mbwembwe za aina aina za kuomba! Lakini kwa nini, au kuna nini vichwani mwa wanyausu?

Kwa nini tusizinduke sasa, mbona wakati tulalamika ukame na umasiki uliokithiri, shemeji zetu Wachaga wanaporomosha majumba ya magari ya kifahari, kwani hivi wanavuchumia wapi! Mbona waheshimiwa kutoka kondoa wanachangamikia tenda, sisi tumebaki “usiku wo monga!”. Haya sasa Vyuo hivyo, wanakuja watoto wa wenzetu wanapata elimu wanarudi kutumikia makwao, hata kama kuna wazalendo wanachuma wanaenda kujenga kwao na baadhi wanawekeza Dodoma.

Wanyausi wana nini, mbona wapo kama wameridhika tu na maisha duni! Tumesikia madinai yalipatikana maeneo Fulani huko Mpwawa wamekuja wenzetu wajanja wakachota, hata huko Wilaya mpya kunatetesi chini kuna mali, badala ya kushiriki midahalo na mijadala mbalimbali nasikiwa wanyausi wameshafyata mkia wao wanafikilia Matembe yao wataenda kuyaotesha wapi!

Wanyausi, Zabibu! Wataliano huko Homboro wanabweda tu, hebu jaribu kuulizia Mvinyo wa Homboro kama utaupata kwa urahisi hapa nchini labla uende majuu Hongera Wanyausi wa Chinangali kuanzisha tena zao la zabibu, lakini angalieni isiewe nguvu ya soda! Kwani hamkumbuki enze za zabibu Mlowa bwani, Kigwe na kungineko vijiji vilinunua mpaka Malori, magari na mashamba hayo vikowapi.

Hongera ndugu zangu wa Mbabala! Kumbe tukiwezeshwa tunaweza, sasa hebu CRDB iingalie na Miradi mingine, kama Ubuyu, unashanga! Hebu tukikusanya maauzo yote ya ubuyu Dalisama tu, mboana watu wanalipa kodi na ada za shule” nkani ya mapela” Mazao kama Alizeti, ufuta na karanga yakiwezeshwa, mashudu tutalisha ng’ombe, na mbuzi wataongezeka mnadani.

Wanyausi, sasa tena hata Nindo, Msunyunto, Muheme, Chipande, Masembegu Chiganda, taja…… hatuvisamini tena, si hata tungetengeneza Single na sisi tukatoka Maanderground! Mbona inawezekana, mbona Dada yetu kavaa koti ya Chimuli akatoka naye alitoka Tanga.

Kaka zangu Mavunde na Yobwa, papa Mchoya yuko wapi? Najua kazi nzuri za huko St. James Arusha, UVUKE-DodoMA, taja.............. Mvua hainyeshi, mbona kumeanzishwa kiwanda cha maji, Sante! Kwani maji ya mzakwe yameisha, mto Bubu vipi sikuizi unaongea, hayo maji tuyafate huko huko chini, Hiviiiiiiii mbona Waarabu hawahami jangwani, sisi kila siku mabasi kwa basi DALISALAMA, tunawaachia wenzetu nyumba, mnategemea nini!

Si ajabu waheshimiwa hawataki kuhamia Dodoma maana wanashanga nyie mnawambia wahamie Dodoma, lakini mnapishana nao Dumila, mkienda Dalisalama, nyinyi mnakimbia nini, halafu mnawazimisha wahamie Dodoma, hiviiiiiii mmesahau usemi wa Wanyausi “Mnyanyumba sangalale……..” Y ako mengi yakusema, lakini iko haja ya wanyausi kufikiria tena, Dodoma tunamwachia nani, Mzee mkubwa, Baba, Koko wewe tu umebaki kati ya Wazee wetu, hivi mkikaa na Mzee mwenzio hamweza kutuamusha, mwene chibede cha chichi! So chi wayangu! Sema neno moja tu mbona tunakuaminia.

Sasa hebu angalia wageni wanakuja sisi tunatoka kwenye vibarua Dalisalama, hata kweli ni adamu ya “KWI KUMBU” tuliojifunzo, ng’o yai! George Kusila alinza kitu cha Wanyausi kuwakumbusha walikotoka, basi hata wakishindwa mengine, miili tu irudishwe ikazikwe kijijini, hata hilo nalo limekuwa gumu, hiviiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Kalumbu asante sana, kwa wasaa huu naomba nikukaribishe kikao cha wanyausi 14/02/2010 Dalisalama , tunapanga sehemu ya kukutana ukinipigia baada ya kesho nitakuwa na jibu.

Wakutya Wagogo chili Chibede, chili machela vitatufikisha wapi ndugu zanguni! Salaam.

from Freddy Kapande (Kigwe) mumbuli@yahoo.com 0715327683

Monday, January 04, 2010

HAPPY NEW YEAR 2010

Nakutakieni heri ya mwaka mpya wa 2010 wasomaji wangu wooote hata wale ambao huwa munapita tu angalau kwa mara chache saaana, nawashukuru sana wote ambao mmekuwa mkitoa ushauri wenu na mawazo mbalimbali na kuifanya webpage hii kuendelea kuishi katika ulimwengu huu wa Utandawazi! Thank U sana all of u!

be blessed Oh!