HAYA ndiyo mambo mbayo huyafahamu
kuhusu wagogo.
Ama kweli
ukistaajabu ya musa utayaona… ya firauni, mila na desturi za kabila la wagogo
bwana kwa mtu ambaye amefariki kutokana na ugonjwa wa kifafa, inakuwaga hivi;
Kwanza akishafariki,ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu hawaruhusiwi kuwa karibu na mwili wa marehemu.
Pili akishawekwa
katika jeneza hatakikiwi kuagwa kwa imani kwamba mtu huyo ni kama najisi Fulani
hivi.
Hii siyo
hadithi jamani mimi mwenyewe ni shuhuda wa tukio hili baada ya mjomba wangu
kufariki kutokana na ugonjwa huo ambao kwa kigogo unaitwa “UTAMWA WA CHINZILISA”. Haya ninayoyaandika hapa ndiyo yaliyotokea katika msiba huo.
Nilishangaa lakini
sikuwa na namna maana ndivyo ndugu zangu wanavyoamini hivyo na hakuna wa kuwabadilisha mpaka siku wafe na
wenyewe.
Baada ya hapo wakishachimba kaburi, mtu huyo hawekwi katika
sanduku ua jeneza kama ilivyo ada kwa dini ya kikristo, na badala yake marehemu
huwekwa katika ngozi na kuzikwa.
Lakini pia sio huzikwa kama marehemu wengine, huyu alifariki
kwa ugonjwa kifafa huzikwa na kila kitu chake, kama vile nguo zake zote, na
ninavyoona kama ingewezekana hata nyumba na vitanda vyake navyo pia anatakiwa
azikwe nanvyo sema ndo haiwezekani tu, LOH!
Baada ya kuzika, hakuna matanga, kinachotakiwa ni watu
kutawanyika na kuendelea na shughuli zao na si vingine.
Ama kweli ukistaajabu ya musa, utayaona ya kigogo, huu nao si
unyanyapaa jamani, ndugu zangu wagogo hebu tubadilike jamani maana haya
mnayofanya kwa madai kuwa eti ni mila yalishapitwa na wakati na wala
hayampendezi Mungu.
Ends………….