HIVI ni Kweli eti kumkeketa mtoto wa kike ni kumfanya asiwe Malaya jamani? Ninauliza hivi nina maana, moja ya mila na tamaduni za wagogo hapo zamani ilikuwa ni kumkeketa motto wa kike ili kumfanya asiwe Malaya.
UNAOBA bwana, unajua kwa nini? Eti wabibi wale wa zamani wanasema kuwa ukimekeketa mtoto wa kike unampunguzia hamu ya kufanya mapenzi na hivyo anakuwa si Malaya!
Sasa sina uhakika kama ni kweli sana, naomba wadau mnisaidie katika hili tafadhali naombeni jamani, naomba mtoe maoni yenu halafu baadaye nitafunga mjadala kwa kuwa bado natafuta materials zaidi ya kuwafahamisha kuhusu mila hii ya mgogo!
Karibuni sana.
kumkeketa mtoto wa kike ni tendo la kikatili ambalo inaaminika na makabila mengi yanayo thamini mila hii kuwa inadaidia kupunguza umalaya.ndio kuna ukweli fulani kwakuwa sehemu inayo keketwa ni sehemu muhimu kwa mwanamke inayo amsha hisia za mapenzi hasa pale inapoguswaguswa.lakini ukeketaji na umalaya ni vitu viwili tofauti kwasababu umalaya ni tabia wala sio ugonjwa wakristo wanaamini ni pepo ambalo liikimwingia mtu anakua malaya haijalishi amekeketwa au la.kuna ushahidi mzuri kuwa ukeketaji hausaidii kupunguza umalaya kwa kuwa hao walio keketwa wamo baadhi ni malaya wa kutupwa.Ninacho jua ,mila ya ukeketaji iliandamana na mafunzo ya maadili mema kwa jamii hii ndio ilipunguza umalaya sio ukeketaji.wagogo katika kipindi hiki cha najando hufunza wahusika jinsi ya kuishi na jamii kwahiyo washiriki hutoka wameiva na kuhesabiwa ni watu wazima na hujitenga na mtu yeyote ambaye hajapitia hatua hata kama ni mkumbwa kupita wao huhesabiwa ni mtoto.mimi nelson chilongani