Thursday, January 26, 2006

KWA STYLE HII, WABONGO MWAKA HUU TWAFA



Hii ndio hali ya Bongo kwa hivi sasa, hakuna pesa hakuna mvua wala hakuna biashara inayofanyika zaidi ya biashara kujiozea na wauzaji kupumzika kwa staili hii ambapo ataamshwa na njaa kali ambapo atakuwa anahitaji menu hiyo hapo kulia, wakati mfukoni hana hata shilingi, jamani tufanye nini wenzenu twafa! tena twafa vibaya maana tutakufa bila ubishi, israeli atatukuta tumepumzika hii ikiwa na maana kuwa tutakufa bila kuugua wala kupata ajali, Ndugu zanguni tumwombe sana mungu atusaidie!!! (picha kwa hisani ya Issa Michuzi)

4 comments:

boniphace said...

Inatia huzuni hii wakati tuliowachagua jana tu wameanza kuomba mishahara lukuki. Soma kwangu kisha msalimie Mustapha aliyekuja na habari hii ya kufungua mwaka kwa siasa za Tanzania za wizi mpya wa kasi na nguvu mpya.

Karibu vibaya kukaa kando kwa mwezi maana tunakumis sana sisi mashabiki zako pale tunapokosa ugali wa mburoguni.

Rama Msangi said...

dada Unatisha sasa...nadhani ndio kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya...jitahidi kaza uzi

Reggy's said...

Hii picha inatisha sana. machungwa yapo tele, lakini soko ndo hakuna. nadhani kuna haja ya viongozi wetu kusisitiza zaidi uwekezaji katika viwanda vya juisi za matunda halisi, ili wakulima wetu waweze kunufaika na jasho lao, badala ya kuvifaidisha viwanda vya ughaibuni. Bye have a nice day

Rama Msangi said...

Famya Ugali nyama 'fulu' hapo basi, kisha nitashushia na chungwa baada ya kushuisha nguna la haja kwa mzee tumbo