Wednesday, March 29, 2006

HAKI ya nani, yaani kweli wabongo sasa tumedata, hebu soma hii kwa makini halafu ufikirie itakuwaje! HAKIMU Mkazi wa Kisutu Jijini Dar Es Salaam juzi Mahakamani aliibiwa gari lake aina ya Suzuki Samurai wakaiti akiendesha Kesi.

Gari hiyo lina thamani ya sh. Milioni 3.5 na aliibiwa akiwa Bize na Masuala ya Kesi Mahakamani hapo.

Hakimu Safari aliibiwa gari hiyo yenye namba za usajili T867 ALA, ambali inadaiwa liliibiwa saa nne asubuhi baada ya hakimu huyo kufika katika eneo lake la kazi na kuegesha.

Baada ya kumaliza shughuli zake za kikazi mahakamani hapo hakimu huyo alitoka nje ya jengo la mahakama akiwa na funguo za gari hilo kwa nia ya kurejea nyumbani na ndipo alipogundua kuibiwa kwa gari hilo.

hakimu huyo alisema kazi kulitafuta gari lake limo mikononi mwa polisi baada ya kuropoti kwa mkuu wa makosa ya jinai (RCO), gODFREY nZOWA ambapo alipatiwa RB namba CD/RB/3147/06.

HII NI KALI KULIKO YA MWANDOSYA AMBAYE ALIVAMIWA KIWA BAA HIVI ALIYEIBA GARI HIYO AKIKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMNI HAPO KWA HAKIMU HUYO ALIYEIBIWA GARI YAKE ANAWEZA AKAPEWA ADHABU GANI???!!!!! INATISHA.

4 comments:

John Mwaipopo said...

Miaka 100 rumande.

Anonymous said...

Mbona nasikia eti utawala mpya umemaliza tatizo la wizi na ujambazi?

Sasa hawa wanamwibia hakimu gari wanataka wawe kama yule hakimu wa Kisutu aliyewahi kupewa "lifti" na mshtakiwa baada ya kesi kuahirishwa kwakuwa hakuwa na usafiri!

Martha Mtangoo said...

Utawala mpya unafanya kazi kupitia katika Vyombo vya habari kila siku rais anauza magazeti mara ooh nimepata majina ya majambazi lakini hakuna lolote ndo kwanza wanaiba kwa NGUVU MPYA, ARI MPYA NA KASI MPYA, kwa hiyo kaka Ndesanjo asikudanganye mtu hakuna cha utawala mpya wala nini huku.

Anonymous said...

huyu jamaa alikuwa anamfikishia ujumbe hakimu kwamba adhabu wanayotoa ni ndogo sana hivyo waongeze au la! alichoka maisha ya uswahilini akahamua amchezee hakimu ikiwa ni njia ya kumpeleka jela fasta fasta