Tuesday, May 02, 2006

Uhuru wa Vyombo vya habari Tanzania Bado ni Ndoto.

Kila mwaka Mei 03 Wanaharakati kote ulimwenguni husherehekea Siku ya uhuru wa Vyombo ya habari Duniani Swali ni Je uhuru huu hapa Tanzania upo au bado longolongo? jadili bila jazba wala upendeleo karibu!!!!!!!!!!!

hivi ndivyo mzee wa sumo na mwenzie walivyoumizwa na askari magereza walipoenda kukava raia wanavyoondolewa kwa nguvu kwenye nyumba zilizokuwa za atc na kununuliwa na magereza kule ukonga. kesi iko inanguruma mahakamani kwani askari jela waliohusika walishtakiwa. Picha na Issa (Michuzi)

9 comments:

Reggy's said...

Usishangae ya Mussa utaona ya firauni. Soma kwangu angalia jinsi waandishi wanavyouawa. Sisi hapa hatujashuhudia, tunasikia tu, kama mambo hayatabadilika, ipo siku...have a good day-RSM-

John Mwaipopo said...

Waandishi kazi mnayo. Tatizo mmezidisha ukweli badala ya uwongo. Yaani hata kaunafiki kidogo haumkajui. Uwongo juu, juu,juuu zaidi.

Jeff Msangi said...

Hii ni vita ambayo huenda isije kuwa na mwisho.Lakini pia ni vita ambayo ina kila sababu ya kupiganwa.

Mija Shija Sayi said...

Martha kumbe na wewe umehama!?..hongera sana.

boniphace said...

Nilichelewa kupita hapa na kisha nikapotea njia. nyumba hii safi sana ama kweli MK Production inatushika hapa mjini kila mtu kujijengea tu na kubadili mandhari. Safi sana Martha kukubali kufanya mabadiliko haya maana yanaendana wazi kabisa na Aazimio la Dodoma, ambalo pia wewe ni muasisi.

Martha Mtangoo said...

Kaka Boniphace na Dada Mija nashukuru sana kwa kunihongera, yaani mmenipa moyo kwa kupenda kazi yangu nashukuru sana wapendwa.

mzee wa mshitu said...

Ndugu yangu Marta au wale kina nani sijui wanapenda kuita Merita (Joke) si utani nilikuwa napita mtaa huu kwa hakika nimepotea nyumba maana imebadilika kuanzi nje hadi ndani. Hongera ndugu yangu haya ndiyo mambo anayofanya huyu mtaalamu wetu MK. huyu bwana inabidi apate tuzo kwa umahiri wake. MK oyeeeeeee! haya kuhusu mabo ya uhuru wa habari bado mno TZ tuna safari ndefu mno kwani kama media imekuwa kisemeo cha serikali unategemea nini.

Rashid Mkwinda said...

Ni safari iso mwisho, kwa waandishi,
Si njema yenye mipasho,haina ucheshi,
Daima ni muwasho,ni ngangari si beleshi,
Uhuru huu ni mwisho,silaha tutahitaji.

Silaha tutahitaji, safari ya kujihami,
Wauawa wanambuji,wajuzi wa hii fani,
Hali watu wahitaji,taarifa makini,
Uhuru huu nimwisho,silaha tutahitaji.

Waandishi kila hali, jicho letu jamii,
Pale palipo zali, hupasha pasi na fii,
Vipi tuzidi kughuri,Tanzania yetu hii,
Uhuru huu ni mwisho,silaha tutahitaji.

Wakatabahu

Anonymous said...

Kasuku ni kweli hamtonyanyaswa maana sasa kuna ile Partisan journalism ambayo inafanya kazi kama vile tupo kwenye ukomunisti, mimi nishaacha kusoma magazeti ya hapa tz afadhaili magazeti tando yana habari kuliko magazeti yanayouzwa mitaani. Kwaa jinsi hii nitanza kusoma magazeti wakati wa kampeni za uchaguzi na taaluma itarudi vizuri nadhani baada ya mika 20, maskini uandishi1 WAANDISHI MNAAMUA KUUZA TAALUMA ZENU KIRAHISI HIVI, mnafikiri IKULU ndiyo inayonunua magazeti! haya kalagha bahoo!