Thursday, October 18, 2007

ALBADIR dhidi ya UbaBE BuNgeNI!!

Baada ya ubabe ndani ya Bunge na kumuondoa Bwana Zitto Bungeni na Bunge kuvunjwa wale wote walio msakama na kumfanyia nyodo wamesha kutwa na haya yafuatayo;

Kwanza alianza Ruth Msafiri wa Muleba Kaskazini. Mumewe alipata ajali mbaya ya pikipiki na kukimbizwa Muhimbili na alifia hapo Mhuhimbili lakini haikutangazwa .

Baadaye Peter Selukamba akiwa anaendesha mwenyewe alinusurika kifo baada ya gari lake kuwa kama chapati yaani ile VX yake ya Ubunge na hadi sasa gari halitamaniki lakini akapona kuumia . Hawakuandika kokote wakafanya siri.

Siku hiyo hiyo Mbunge Malima akiwa anaendesha yeye mwenyewe akapata ajali pale uwanja wa JK Nyerere akanusurika kuumia lakini gari inahitaji matengenezo makubwa waandishi wa majira kimya hawajasema lolote . Baadaye akaja Mudhihiri wote mnayajua ya kwake.
Juzi kapata ajali mbaya sana ndugu Kumchaya Selemani wa Lulindi.Watu 2 wamekufa na yeye kanusurika .

We all have also heard about Juma Kapuya ……

Je hiki ni kitu gani ? Mungu kutupigania Watanzania ?

Je kwa nini vyombo vya habari visiandike? Au Albadir ilyosomwa na watu wa mwisho wa reli si mchezo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani waheshimiwa kuweni makini wakati wa kuongea maisha haya huwa mafupi pale yanapoanza kuwa matamu!

Saturday, August 18, 2007

KUMUMUVUZISHA ZITTO KABWE KUMEMPANDISHA CHATI, SASA YUKO JUU


KUMUMUVUZISHA Zitto Kabwe, Kumempandisha Chati, sasa yuko Juu!!!!!



Kama Wabunge waliounga mkono Mh. Zitto Kabwe asimamishwe walifikiri wanamkomoa, basi hali ni tofauti kwani wananchi kibao wamemuunga mkono.


Baadhi ya Wabunge wakichangia mjadala wa kumsimamisha walisema anatumia Bunge kujipatia umaarufu wa kisiasa kumbe wenyewe ndio wanampatia umaarufu kwa kumtimua.Wananchi wengi wamechukizwa na kitendo cha kumsimamisha Kabwe kwani wanahisi ni janja ya kuwafunga midomo baadhi ya Wabunge wenye nia ya kweli ya kufichua maovu.


Kuanzia wasomi wa Chuo Kikuu (Profesa Mwesiga Baregu, mhadhiri mwandamizi wa masuala ya siasa na ushirikiano wa kimataifa wa UDSM) wamesikitishwa na uamuzi huo wa Bunge.Prof. Baregu alisema kwa kitendo hicho, Bunge halikumtendea haki Kabwe, halikutenda haki kwa demokrasia na pia halikutenda haki kwa wananchi.


Alisema kumwadhibu mbunge huyo hakujaweza kuondoa ukweli kwamba kuna mikataba mibovu inayoingiwa na serikali na suala la Buzwagi ni mfano tu kati ya mikataba mingi mibovu iliyoingiwa, hasa ya madini.


Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila pia ameungana na wenzake akisema Zitto hana kosa, adhabu aliyopewa ni uharamia wa demokrasia na suala ambalo kila Mtanzania anatakiwa kulitambua na kutotakubali kukaa kimya.


Naye Wakili wa Kujitegemea, Tundu Lissu, alisema adhabu iliyotolewa kwa Kabwe sio halali, huku akitaka mbunge huyo aruhusiwe kuendelea na vikao vyote vya Bunge.Akiongea kwa niaba ya Asasi za kiraia Lissu alisema ni bora Bunge likaeleza mbunge huyo amepewa adhabu ya ngapi ili wananchi walinganishe na kufahamu adhabu ambayo ilikuwa inastahili kulingana na kosa, kama analo.


Wengine waliohojiwa wamesema uamuzi huo ni sawa na kuwanyima haki wapiga kura wa Kigoma Kaskazini kwani watakosa mwakilishi kwa kipindi alichosimamishwa.Hivi sasa Mbunge huyo anawasiliana na baadhi ya wanasheria kuona uwezekano wa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga adhabu hiyo.


Na katika kumwuunga mkono CHADEMA wanaandaa mapokezi ya Mbunge wao huyo pindi atakaporejea Dar akitokea Dodoma alikomuvuzishwa nje ya Bunge hadi Januari mwakani.


Huko Dodoma nako Wabunge wa upinzani wamekaa kikao cha dharura kutafakari cha kufanya baada ya mwenzao Kabwe kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge.Na katika kumuunga mkono Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa kila mwezi watakuwa wanamchangia karibu sh. milioni 1.5/- ili afanikishe kazi zake anazofanya za Ubunge.Katika adhabu aliyopewa Mbunge huyo atakuwa analipwa nusu mshahara hadi atakaporejea tena Bungeni kuendelea na vikao.

Friday, February 02, 2007

MLIOKO UGHAIBUNI WENZENU HUKU HALI NDIO IKO HIVI!!!!

JAMANI HUKU WENZENU HATUSAFIRI TENA!

Huu ni Msafara wa Naibu Waziri wa Miundombinu Dk. Milton Mahanga ambao ulikwama katika eneo la Isuna Mkoani Singida wakati akikagua barabara ya Dodoma-Manyoni, Manyoni-Singida, huku hali ni mbaya sana jamani wasomaji wangu na hasa nyie mlioko Ughaibuni akina Macha Ndesanjo. zaidi ya shilingi bilioni 45 zinahitajika kukarabati barabara hizi ili kurudi katika hali yake ya kawaida.