Friday, February 02, 2007

MLIOKO UGHAIBUNI WENZENU HUKU HALI NDIO IKO HIVI!!!!

JAMANI HUKU WENZENU HATUSAFIRI TENA!

Huu ni Msafara wa Naibu Waziri wa Miundombinu Dk. Milton Mahanga ambao ulikwama katika eneo la Isuna Mkoani Singida wakati akikagua barabara ya Dodoma-Manyoni, Manyoni-Singida, huku hali ni mbaya sana jamani wasomaji wangu na hasa nyie mlioko Ughaibuni akina Macha Ndesanjo. zaidi ya shilingi bilioni 45 zinahitajika kukarabati barabara hizi ili kurudi katika hali yake ya kawaida.

11 comments:

MTANZANIA. said...

Martha nimekupata. Ama kweli hali hii inasikitisha ukizingatia kwamba ni zaidi ya miaka 40 toka tupate uhuru na bado mambo si hwari. Anyway napita kujitambulisha na karibu sana kwenye blog yangu.

Unknown said...

Martha ulipotea muda mrefu.leo nilipita kuchungulia tu nikakuta wenyeji wapo.haya poleni na matope.unajua tatizo ubovu hizo barabara hauwasumbui wanasimamia ujenzi wake.huyo mheshimiwa hata gari yake ikikwama yeye hayumo katika timu ya wasukumaji!

Anonymous said...

Martha, ulitukimbia kabisa, tena bila taarifa. Karibu ulingoni.

Hizo barabara kwanini zisijengwe na wale waliohusika na ununuzi wa rada?

Simon Kitururu said...

Duh!Kasheshe!

Rama Msangi said...

kaaazi kweli kweli.
Hivi kulikuwa na busara gani mamilioni ya wananchi kutumika kwa ajili ya kujadili suala la watu wawili tu sababu wana fedha zao, badala ya fedha hizo walau kununulia mchanga kwa ajili ya kuandaa barabara hiyo? Watu wanatumia pesa zao katika kulumbana, serikali inatumia pesa za wananchi katika kuwajadili, barabara zinabomoka.

shughuli kweli kweli hiyo

Egidio Ndabagoye said...

Aisee! Ndesanjo huogopi eti nini?Rada?
Ile barabara ya Shekilango vip inaendelea kweli?

Martha Mtangoo said...

jamani kaka rama unajua nini, wale jamaa wa SIetco WANAOJENGA BARABARA YA mANYONI sINGIDA, WANA HALI MBAYA SANA YAANI NILIWAONA NIKAONA HAINA MAANA TENA KUENDELEA KULIPA KODI YANGU UNAJUA WANATIA HURUMA MDA MWINGINE WANATIA HASIRA, POLENI SANA WASOMAJI WANGU NIKO SHULE MDA MWINGI!

Rashid Mkwinda said...

Kilichopo ni usanii, wa wale wanaopenda kula mafungu ya walipa kodi, ununuzi wa rada, ndege ya RAHISI ikiwa ni pamoja na kujadili suala la MALI-MAA na MEENGI na baada ya kugundua kuwa MALI--MAA kalonga uongo akasamehewa na SUPIKA wa BUU LA NGE bila kujali kwamba tume iliyoundwa imetumia mamilio ya fedha kuchunguza suala hili.

Huwa nacheka sana,nikikumbuka yule jamaa wa Kiraracha alipoomba msamaha bungeni asamehewe kutokana na kusema urongo ndani ya bunge enzi ziel akiwa ni Mbynge wa Temeke kupitia TLP kama sikusahau hivi huyu kw akuwa alikuwa kambi ya upinzani na huyu wa Chama twawala?sipati PIKCHA

Anonymous said...

Jamani pesa na misaada yote serikali inayopatiwa kweli wanashindwa kujenga barabara nchini? Hicho ndio kinachotufanya tusirudi Tanzania ingawa Kikwete anakuja kutubembeleza turudi kujenga nchi yetu, pesa yote inaishia matumboni mwao

Anonymous said...

Wanunuzi wa rada wajenge hizo barabara.

Msomaji toka UK

Anonymous said...

Martha nafurahi unatupatia hali ya barabara zetu za nyumbani. mara ya mwisho njia hiyo nilipita mwaka juzi, tokea Misigiri hadi Sekenke barabara iliharibika sana, wakandarasi walikuwa bado wanatambaa kutengenza. kumbe hali bado mbaya, bora Mkapa arudi atutengenezee . pia badilisha picha hapo juu, inatuumiza macho . Sally TEXAS