OO! mziki wa kizazi kipya unakua! unakua kwa vigezo gani? hebu anganlia mambo yanayofanywa na wasanii hao halafu uchangie unakua kwa vigezo gani na kiwango kipi!
kwa nini iwe mbele tu? na siyo Kwenye mataa ya Koo? kwa nini washike mbele tu tena kwenye nanihii na isiwe mgongoni au kuyakumbatia kabisa mabega?
kwa nini wasanii hawa hupendelea kushika sehemu za siri na kuziminya kana kwamba zimewakosea kwa kiasi kikubwa na wanatoa adhabu?
ndivyo mziki wa kizazi kipya unavyokua kwa kufanya mambo ya ajabu ajabu tena kwa kuiga toka kwa akina P. Diddy na wenzie kina Snoop DogDog.
Ina maana akina P. Diddy wakila V-nye-C na wao watakula vya kwao? hayo si ndo mambo ya kuiga? si twaigan kila kitu toka magharibi? Wao washike nasi tushike ? wao wakisema Maza faka nasi twasema baza faka!
wakitembea mataa ya koo nje nasisi tutembee mataaa ya koo wazi eti tu kwa kuwa P. Diddy kaacha yake nje? utamaduni huu umeanza lini kwetu Tanzania?
Mjinga atakwambia huu ni ushamba, kwani mkiimba huku mnapeperusha mikono kama mnataka kupaa mbinguni bila kuipeleka kusini mziki hautachezeka?
Si mshike basi hiyo maiki kwa mikono mikono miliwi? mbona kuna staili nyingi tu za kucheza vizuri bila hata ya kumsumbua huyo jamaa?
kama mmeshindwa kubuni staili nyingine ni bora tu muwe wastaarabu kama mnacheza ngona ya Mganda maana hii ndiyo asili yetu watanzania.
huu ni ushauri wa bure kwenu nyie vijana wa vizazi vipya, kama hamtaki mtajiju, na kushikashika kwenu huko WALAH! mtajikuta siyo ridhiki!
Mnadhani huyo jamaa anapenda kuchezewa ovyo? Mazingira, tamaduni na makuzi yetuhayako hivyokizazi kinateketea kimaadili huku wanajua kuwa wanayoyafanya si mema machoni pa watu.
makabila mengine wanapoona mnashika hivyo kwao tafsiri yao ni matusi makubwa ya nguoni sasa mnafikiri watakuja hata kwenye hayo matamasha yenu watukanwe?
Badilikeni basi vijana wenzangu kwa kuwa huo mziki wenu hata mimi naupenda sana lakini naogopa kutukanwa pale mnaposhika chini, acheni kumfundisha Junior Tabia mbaya.
wasanii wa kizazi kipya na kile cha zamani bila kuwasahau wasomaji wote mnakaribishwa kutoa maoni yenu bila jazba wala upendeleo wa aina yeyote karibuni sana!
2 comments:
Hakyanani mtani ninaye loooh!!!!
Hebu waambie maana wasijelaumu wakigeuka...si rizki...
Huu ni aina nyingine ya upuuzi ambao tumekuwa ukiuiga toka kwa wenzetu. Ukihunguza sana sio ajabu ukajua kuwa mtu wa kwanza kufanya hivi alikuwa msanii toka Ulaya na alikuwa amekatikiwa na mkanda (wa suruali)siku hiyo, akajidai kuzuga kwa kufanya ni fasheni kumbe wenzake wamepata ha kuiga. Iko siku tutaia hata isiyoigwa na wala sio mbali ni karibuni tu!!!
Post a Comment