Friday, October 28, 2005

AKIFA Mwingine uchaguzi si utafanyika 2006? Mrema naye Hoi kitandani!

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jana imetangaza kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kufuatia kifo cha aliyekuwa Mgombea urais Mwenza wa CHADEMA kufariki dunia.

NEC imetangaza tarehe mpya ya uchaguzi kuwa nui Desemba 18 mwaka huu kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

nilipopata tarifa hizo jana nilishtuka sana kwa maana kwanza huyo mgombea mwenyewe ukweli nilikuwa simfahamu kabisa kwa jina wala kwa sura, ushanipata bwana?

unajua kitu gani kimenishtua ni hiki: uchaguzi umeahirishwa hadi Desemba 18 mwaka huu, eti mpaka CHADEMA wateue mgombea mwenza mwingine wamnadi halafu ndo watu wampigie kura!

unajua inachekesha sana, panapochekesha ni hapa: huyo marehemu mwenyewe ni watu wangapi walikuwa wanamfahamu? na je huyo atakayeteuliwa atapa kura ngapi?

haya muda nao sasa akifa mwingine itakuwaje? maana mrema naye ambaye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TLP ni mgonjwa hoi bin taaban kitandani! kwa kweli tume imenichanganya sana.

kwanza wagombea wenyewe wamechoka na kampeni, lakini pia hata sisi wananchi pia tumechoka, cha msingi sasa ni mara bunge litakapopatikana itabidi libadilishe sheria zote zilizopitwa na wakati ikiwemo hii sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 maana imenichefua sana.

zisiporekebishwa Serikali yenyewe itajikuta siku moja inajifunga na sheria iliyotunga yenyewe na mbaya zaidi mpaka sasa jumla ya sh. bilioni 43 zimeshatumika kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, ambapo jumla ya sh. bilioni 93 zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi huo ambao sasa utafanyika Desemba 18.

Mimi nimechoka sana na siasa za inji hii sijui nyie wenzangu mnazionaje?

6 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Wengine tumechoka na hawa wezi waliopo madarakani kipindi hiki.
Tumewachoka!!!!

boniphace said...

Suala lililopo hapo si kubadili sheria za uchaguzi ni kufuta katiba na kuandika mpya maana iliyopo ni butu na haina dira ya kuongoza watu kufikia maendeleo ya dunia ya sasa. Kama tumeshindwa tuishi kama Uingereza bila kuwa na Katiba iliyoandikwa.

Anonymous said...

this is all but gay

Anonymous said...

MWEZANGU WEEEE,hujui kama watu hao ndio wanaoilinda hiyo katiba ili wawezekula na kusaza.kwani hujui kama huko kualishwa kwao kuna manufaa makubwa tena isitoshe wanaombea hata huyo mwingine mwenye kujitia anauchungu na inji hii atangulie na vizibiti vyake vya magazeti mimi sina lakusema ila naoba mungu aniweke mpaka pale nitakapo ona watanzania watakapokuwa na kaulimoja nasijui kitakuwa nini!!?

mloyi said...

Kwani sheikh Yahaya hakutabiri? Mkapa atapata kipindi cha tatu kinyemela ambacho kimeshaanza.
Katiba inaruhusu hivyo tusiwe kama CUF wanaingia kwenye uchaguzi wakishindwa wanaandamana kwamba katiba imewanyima haki. kwanini wasiandamane kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mfumo wa uchaguzi ubadilishwe?
Muafaka ulifikiwa tume huru ya uchaguzi ikapatikana lakini mpaka leo tume bado ni CCM, tujaribu kuwaiga wamarekani kwa hili.

Innocent Kasyate said...

Martha umegusa roho yangu unajua hili si tatizo la TZ tu. Hapa Uganda wamebadili katiba ili kumsaidia mtawala akae madarakani maisha.
Mimi nafikiri tunahitaji katiba mpya kabisa.
Tumekwisha.