Thursday, October 13, 2005

Kha! Kumbe Nchi Imeshaposwa? Wenye Nchi tunafanyiwa Kicten Party Sasa!!

HAKI ya Mungu sasa Tanzania tunakoelekea kubaya sasa, Ni jana tu nilikuwa nasoma Blog ya Bw. Msangi nikakutana maoni ya Watu wengi sana kuhusiana na Matunda ya Uhuru ambaye kwa sasa yamegeuzwa Matundu ya Uhuru!

kilichonishtua zaidi baada ya kusoma maoni ya msomaji mmoja ambaye alisema kwa sasa Tanzania imeshatolewa Posa na Wawekezaji toka nje ya Nchi ambao kabla ya kuioa Tanzania bado wanaifanyia Kitchen Party!

Mbaya zaidi waowaji hao wanakuja na mashartimagumu sana kwa waolewaji jambo ambalo linawakandamiza sana waolewaji lakini cha kujiuliza ni hiki je ni Kweli Tanzania haina uwezo wa kutafuta vitendea kazi vyenye ubora wa kimataifa na kufanya kazi zake yenyewe na kuwauzia haoa hao wanajiita wawekezaji?

Najisikia hasira sana ninapoona Mkurugenzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita ni Mzungu wakati kuna watanzania ambao wana uwezo wa kufanya kazi hiyo ya Ukurugenzi katika Mgodi kama huo.

Sasa sisi watanzania ambao tunafanywa Mali Ghafi tufanye nini ili Tusikandamizwe na hawa waowaji wenye masharti Makali namna hii?

5 comments:

mwandani said...

Ndugu yangu mwenzako huwa naangalia na kusikitika na Bongo yetu.
Basi kuolewa sio makampuni ya migodi tu, hata wahudumu wa migahawa, maafisa wa serikali, mpaka mabinti na mijidume. Miye nilishawahi kunyimwa huduma bongo wakati mzungu alihudumiwa nikiona pale pale, nikazua zogo wakaitwa polisi, ikabidi nikimbie kama mwizi, kulala mazabe mie aka!
Mpaka tuweke mguu chini dada yangu na kukataa.Vita mbele.

Rama Msangi said...

Kazi nzuri sana dada. Mara nyingi nimekuwa najitahidi kujiuliza hivi hawa ni WAWEKEZAJI au WAEZEKAJI? Kwasababu wanakuta misingi yote ya miradi hiyo imekamilika wanakuja tu kuitekeleza, lakini wanapofanya hivyo basi wangekuwa wanatujali lakini wao mmmhhh.

Yaani ni kama mtu akukaribishe chakula kizuuri kwake na ukishaanza kula ili kumwonyesha kuwa umeshiba unaanza kumshushia mashuzi ya ajabu ajabu.

watambue kuwa tutafumba pua zetu kwa muda tu na sio daima, siku uzalendo ukitushinda, WATALIJUA JIJI

Indya Nkya said...

Tatizo ni kwamba wote tumeshauzwa ndani ya nchi. Yaani wote ni mali ya wajamaa waezekaji- nikope msemo wa Msangi. Mambo yote yanaamuliwa Washington. makampuni makubwa ndiyo yanaendesha nchi. Aha!!!

Ndesanjo Macha said...

Ndio maana nasema umefika wakati wa kuipiga sirikali marufuku. Au sio?

Innocent Kasyate said...

Tatizo ni kwamba hata kabla ya uwekezaji kuja tuliuwa kila kitu.Watu wametajirika hatutaki kuwawajibisha ndio hao hao tunawapigia kura kila kukicha, sasa tumeamua tuweke wageni tunalalamika pia.Inanichanganya sana manake inaonekana ni bora wezi wa ndani kuliko wa nje.
Kwangu hali zote ni mbaya.Hapa inabidi tuanzishe taifa upya, tukae chini tufikiri manake hawa jamaa wa Washington wametugundua na wametutia kitanzi;hatuna ujanja tumekwisha.