Saturday, December 10, 2005

Hii ndio Hali halisi ya Wabongo!!!!!





HII ndio hali halisi ambayo inatukuta wabongo wengi hapa kwetu, kagari kadogooo lakini watu kibao, utadhani marobota ya Pamba yanasafirishwa toka shinyanga kwenda Dar es salaam kwenye kiwanda cha kutengenezea Nguo.

halafu mbaya zaidi gari hii ikakosa mafuta na kuna watu wana haraka zao wengine wagonjwa, wengine wanawahi Benki kuchukua hela kwa ajili ya kununulia mahitaji yao na mbaya zaidi siku yenyewe ni ya Jumamosi ambayo ni nusu siku!

safari moja huanzisha nyingine, yalishamkuta Mgombea urais Mwanamke Pekee , Komando Anna Senkoro mara Wese si likamuishia!!!!!!!!!!!!!!!!! basi bwana akaanza kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Mafuta kama CHAMA CHA MADAKTARI WANAWAKE (MEWATA), wanavyoomba kuchangiwa fedha kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya matiti kwa akina mama!

sasa mbaya zaidi ni kwamba pamoja na gari hili kujaza watu kibao babaake! sheli hakuna wese wala nini ili kuepuka usumbufu kwa wafanyakazi kuulizwa mafuta yapo? wameamua kuweka Bango Kubwaaaaaaaaa, Eti NO FUEL! UNGEKUWA WEWE NI MMOJA WA ABIRIA KATIKA GARI HII UNGEFANYAJE?

Nakaribisha maoni, changia bila jazba wala upendeleo!

10 comments:

Jeff Msangi said...

Ningekuwa mimi abiria ndani ya gari hilo ningeshuka na kujaribu kutafuta utaratibu mwingine.Na penye nia pana njia.
Anna Senkoro anafanya jambo la maana sana katika kukuza demokrasia.Ningekuwa karibu naye wakati anachangisha hela za mafuta ningemsaidia kama ningekuwa nazo.Chama cha madaktari wanawake wanahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote.Jamii za huku nilipo mimi zinaendelea na kuendeshwa na michango inayotokana na harambee kama hizo.Saratani ni ugonjwa hatari sana.Ningefurahi kama ungetoa kiunganishi cha hicho chama cha madaktari wanawake ili wenye uwezo wakichangie!

Martha Mtangoo said...

Nafurahi sana kuona watanzania wenzangu walioko nje ya Tanzania wanakuwa na moyo kama wako, niandikie kila unachohitaji kwa ajili ya kuchangisha na kutuma michango kwa ajili ya mewata nitakupatia, tumia Email Yangu, mmtangoo@yahoo.com, nani kama mama?

Mija Shija Sayi said...

Ningetoa kilongalonga changu nikampigia mgombea yeyote wa ccm aje na pajero lake atufikishe tuendako, ninahakika asingekataa. Huku nyuma tungejipanga kwamba akifika ni ama zetu ama zake. Ni lazma tumweke kati atueleze kiunagaubaga...Inakuwaje yeye na wenzake wanakuwa na Mapajero na hawaishiwi na mafuta? ...halafu akina sisi hata tufurukute vipi katika maisha tunaishia mikweche kama hii tena kwa petroli ya mgao?

Kasheshe isingeishia hapo, tungemnyang'anya lile Pajero na kumkabidhi ule mkweche...sasa yeye ndio angejua wapi atapata petroli.
Alaa!

Ndesanjo Macha said...

Nina tabia ya kucheka wakati mwingine wakati ambapo jambo lenyewe sio mzaha. Mishipa yangu ya kicheko iko karibu mno. Nilipoona picha hizo (hiyo inayosema kuwa spesheli ya mwezi ni kuwa hakuna kiwese!, na hilo gari ambalo dereva au mwenye nalo hawalipendi kabisa).

Nami sikujua kuhusu chama hiki cha madakitari wanawake. Tafadhali kama wana tovuti tupatie.

Ndesanjo Macha said...

Nina tabia ya kucheka wakati mwingine wakati ambapo jambo lenyewe sio mzaha. Mishipa yangu ya kicheko iko karibu mno. Nilipoona picha hizo (hiyo inayosema kuwa spesheli ya mwezi ni kuwa hakuna kiwese!, na hilo gari ambalo dereva au mwenye nalo hawalipendi kabisa).

Nami sikujua kuhusu chama hiki cha madakitari wanawake. Tafadhali kama wana tovuti tupatie.

Semkae said...

Ndiyo maisha ya bongo hayo. Home ni home lakini.

Njo muone picha zenu.

http://pichazenu.blogspot.com/

Anonymous said...

mh!
kwa hakika ni zaidi ya nifikirivyo kwa picha nionazo za Bi Anna Senkoro,unajua gari yake na mambomengine yeye na BIBI titi MoHAMMED ni sawa kwa kuwa wapo kwenye ulingo wa sihasa hizi hizi,sema moja alikuwa zama za (julius kambarage)JK senior na mwingine(jakaya Kikwete) JKjr
tena naona historia inaweza ikamtambua kwa vituko hivi kwa kuwa ni wa kwanza mwanamke kugombea urais,tena ktk hali duni,na zaidi ya yote akashindwa hata kufka chalinze kufanya kampeni

Reggy's said...

hizo picha zikuzishangaa hata kidogo, kwa sababu nimezizoea. daladala za kwenda kwetu kule Kamachumu, zinajaza hivyo hivyo na abiri wengine wanakaa kwenye carrier. waliowahi kukaa bongo hamjawahi kuziona! sasa mnashangaa nini?

Innocent Kasyate said...

Kama unajua sehemu inaitwa Kirua Vunjo basi nenda kule Moshi ulizia, ndio kwetu huko. Magari kama hayo ni kawaida manake barabara zetu kule basi au vipanya haviendi kabisa.
Nasikia wamenchagua mbunge wa CCM labda atasaidia manake tumekuwa na wapinzani kwa miaka kumi bila mafanikio.

Martha Mtangoo said...

Naomba nikushukuruni sana wasomaji wangu na wanablog wenzangu pia, naona kila mtu ametoa maoni yake bila jazba wala upendeleo, ok nakutakieni kila la kheri na kazi njema, na kwa maneno hayo machache natamka kwamba mjadala huu umefungwa rasmi! akhsanten.