Monday, June 12, 2006

HAPA NI MHESHIMIWA MBUNGE NDO KAVAA HIVI JE ALIPOKUWA PAPARAZI KAMA MIMI ILIKUWAJE?????!!!!!!!!


MHISHIMIWA AMINA CHIFUPA MPAKANJIA(CCM)!!!!!!!
HAKI YA NANI, INASEMEKANA MBUNGE HUYU NDIYE ANAYEONGOZA KWA KUJIRUSHA KULIKO WABUNGE WENGINE AKIFUATIWA NA BIBIE HALIMA MDEE MBUNGE WA VITI MAALUM (CHADEMA). MBUNGE MWANAUME ANAYEPENDA KUJIRUSHA NA MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WENGINE BADO SIJAMPATA KAMA KUNA MTU ANAFUNUNU HIZO BASI ANITONYE!

10 comments:

mloyi said...

Sijui hawa jamaa huwa wanaangalia vigezo gani kwenye kumpa mtu ubunge! Angalia heshima ya ubunge na jinsi wanavyochagua mbunge asiye na mwelekeo wala maadili, hivi wanategemea nini toka kwake!. Labda kuendeleza muziki wa kizazi kipya, kwa njia ileile inayowafanya wengi waupigie makelele ya kuupinga au kuvaa vi-top ambavyo ni kero kwa wengi- waumme kwa wake- na kuunda makundi ya ajabuajabu kama 'al-quida sisters'.
Najua hayuko peke yake, mwingine mwanaume ana tumbo kubwa nilimuona posta amevaa jinzi kama mcheza shoo wa twanga au bakulutu.
Tujiangalie tunakoenda.

Anonymous said...

Kwanini sisi Waafrica tunafikiri mwanamke mzuri hawezi kuongoza nchi?

Rashid Mkwinda said...

Mie nadhani kungeanzishwa Miss Parliament ili waheshimiwa wabunge nao wawe na uwakilishi kama hivi ndivyo ilivyo kwa Mheshimiwa Chifupa, lakini mimi nadhani umri nao unachangia, tumvumilie hadi afikishe japo miaka 30 huenda atajirekebisha mwenyewe automatically,lakini jamani wacha tuseme hadhi ya bunge letu la Tanzania inataka kushuka hususan kwa hawa wabunge ambao si ridhaa ya wananchi(waliopitia huruma ya kuteuliwa)

Nalitolela, P. S. said...

Naomba nijibu hoja ya dada Mirian hapo juu. Nadhani wanacholaumu watu sio uzuri wa Mh. Chifupa wa Mpakanjia. Wanachosema watu kuwa kutokana na hadhi yake sasa kama mbunge inabidi achague mavazi anayovaa, na pia shughuli mbali mbali anazohudhuria na kiwango cha kushughulika kwake.
Binafsi vazi alilovaa katika picha hii sioni kwamba ni baya sana, lakini sidhani kama utakuta mbunge mwingine duniani kavaa vazi kama hilo. Unapochukua nafasi kama hiyo inabidi ukubali kuwa una majukumu kwa jamii na hivyo inabidi uweke heshima fulani mbele ya macho kwa watu, na hivyo basi lazima uwe tayari kupoteza uhuru kidogo wa kuchagua mavazi, starehe unazozifanya, n.k.

John Mwaipopo said...

Mtasema namuonea-ga wivu Mheshiwa sana Amina Chifupa. hapana. Ana matatizo mawili ambayo mjumuiko wake ndio unaozaa matunda haya tunayoyaona. Moja ni umri mdogo (bado mtoto tu) la pili ni elimu ndogo. Bungeni kuna wenye umri mdogo kama Amina laini elimu ya kutosha. Wapo pia wenye umri wa kutosha lakini elimu bahati mbaya. Lakini makundi haya mawili niliyoyataja hakuna ambalo mapepe kama huyu mdada. Anahitaji kufundwa kielimu kidogo midhali uwezo wa siasa anao. Ingekuwa vipi hata 'rede' atacheza sasa hivi huyu

Anonymous said...

Mimi sioni Tatizo lolote kwa Amina..oops Mheshimiwa Amina,au Mheshimiwa Halima Mdee kujirusha. Wakiwa kama binadamu wengine wowte wanahobi zao,na kwa bahati mbaya au nzuri Bi Halima yake ni kujirusha, mwacheni ajirushe,muda wake wa kuvaa hijabu ukifika atavaa hijabu mpaka mshangae.
Katika upande wa Mavazi,naweza kuungana na wengi,kwa kuwa bibie huyu ameshaukwaa Uheshimiwa lazima na mavazi achague ya uheshimiwa vilevile.
Ila mimi kinanishangaza binti kama huyu kuandamwa kama anavyoandamwa na kuonekana kama mtu asiyekuwa na maadili kwa hadhi hiyo ya kibunge.
Kumbukeni msemo wa avumaye baharini... bunge letu la Tanzania linanuka kimaadili,kipindi cha bunge hapo Dodoma huwa kama sodoma na Gomora,kiufupi wabunge ni Malaya sana,hao wabunge wa jinsia ya kiume baada ya Bunge hawafikirii mambo yoyote zaidi ya pombe na ngono na tatizo hawachagui changudoa yeyote wanapitia, wanafunzi nao wanawapitia then wanarudi wanatongozana na wabunge wenzao wa kike,na mifano hayi ipo... si mnaikumbuka ndoa ya Bwana John na Bi Kilango.
Sasa kama kupiga kelele wabunge wote wapigiwe kelele si Amina Pekeee

Anonymous said...

NAONA WACHANGIAJI WENGI WAMEPUNGUKIWA.HAHT WEWE ULIYETUWEKEA PICHA HII UNA WALAKIN.HIVI JAMANI ELIMIKENI KIDOGO.KILA VAZI NA MAHALA PAKE ATI.HIVI AMINA AJIZEESHE KISA NINI UHESHIMIWA?!LOH SALALE,HESHIMA YA MTU NI YEYE MWENYEWE ANAVYOJI PRESENT MBELE ZA WTU.AMINA IS GOOD LKN WATU WANAMCHUKIA SANA.MTAKUFANACHO SHENZI NYIE.VAENI NYIE BAIBUI DISCO MHESHIMIKE,MAFALA WAKUBWA.AMINA ANAFANYA MAMBO MAKUBWA KUSHINDA HATA UMRI WAKE,NAMPONGEZA.HUREEEEEEEEEEE DA AMINA!!!!

Anonymous said...

Kazi ya ubunge ni sawa na kuongoza jamii. Mbunge lazima awe mfano mzuri katika jamii.

Mama Malaika
UK

Anonymous said...

kwa kumbukumbu zangu finyu, Amina alipiga picha hii kwenye harusi ya Gadner G Habash na lady jay dee, militaka avaeje? je wakati huo Amina alikuwa tayari ni mbunge? na kama alikuwambunge mlitaka avae nini kwenye harusi, gunia?

Anonymous said...

MIMI NAPENDA SANA MAPIGO YA HALIMA MDEE PIA HUWA NAFURAHI KUMUONA AKIWA BUNGENI KWELI ANAVAA SURA YA KAZI KWA HUMAN CHANGE ACCORDING MAZINGIRA SO MDEE BIG UP MY YOUNG SISTER
ballyathanas@hotmail.com