Tuesday, December 02, 2008

Jamani ee wauza nyama Dodoma wametugomea tena wenzenu , tukitaka nyama mpaka twende Dar es Salaam!

JAMANI mlioko ughaibuni huku wenzenu karibu na waume zetu wanagoma ndani ya nyumba sijui itakuwaje, baada ya migogomo kufanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini zikiwemo sekta nyeti kabisa, hatimaye wafayabiashara wa Ng'ombe na uchinjaji wamegoma kuchinja ng'ombe kwa muda usiojulikana, kwa maana hiyo Dodoma hatuli nyama tena hadi watakapoamua sijui itakuwa lini hiyo, hebu Jimuvuzishe hapa kwa habari zaidi!

Na Martha Mtangoo, Dodoma

12/2/2008

UMOJA wa wafanyabiashara wa uchinjaji Ng’ombe Dodoma, (UWANDO), wamesitisha huduma ya kuchinja Ng’ombe na kuuza nyama kutokana na kupandishwa ushuru katika machinjio ya kisasa na hivyo kuufanya mji wa Dodoma kukosa nyama kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara hao wamepandishiwa ushuru kutoka sh 10,000 waliyokuwa wakilipa awali hadi kufikia sh 20,000 kwa ng’ombe mmoja kuanzia juzi.

Wakiongea na waandishi wa habari jana katika eneo la mnada wa mifugo wafanyabiashara hao walisema kuwa walikuta tangazo juzi katika machinjio ya kisasa kuwa kuanzia juzi wanatakiwa kulipia huduma ya uchinjai y ash 20000 kwa kila Ng’ombe.

Mwenyekiti wa UWANDO Taita Ikoyi, alisema kuwa baada ya kuona tangazo hilo walishtushwa na kuamua kusitisha uchinjaji wa Ng’ombe kutokana na gharama za uchinjai kuwa kubwa ikilinganishwa na bei ya mifugo ilivyo sasa.

“Sisi hatujagoma ila tumeamua kusitisha huduma ya kuchinja mifugo yetu na kupeleka nyama katika mabucha kutokana na bei ya ushuru kuwa kubwa, tunabebeshwa mzigo mkubwa sana tunaiomba serikali itufikirie na sisi wadau itupunguzie ushuru” alisema Taita.

Naye Katibu wa UWANDO, Charles Laizer alisema kuwa tangu kujengwa kwa machinjio hiyo ya kisasa wamekuwa wakilazimishwa kupeleka mifugo yao kwenda kuchinjwa katika machinjio hiyo jambo ambalo limekuwa likiwakandamiza mno.

Laizer alisema kuwa awali baada ya kuanzishwa kwa machinjio hiyo walielezwa kuwa kuna uchinjai wa aina tatu ambapo moja ya uchinjai huo ulikuwepo ule wa kawaida kwa wafanyabiashara ambapo walitegemea uchinjaji huo ungekuwa wa bei y ash 1500 kama ilivyokuwa hapo awali lakini imekuwa tofauti na matarajio yao.

“Kama hali yenyewe ndio hii ni bora manispaa ijenge machinjio nyingine yenye ushuru wa bei nafuu na sisi wadu pia tuko tayari kujenga machinjio yetu ilimradi serikali itueleze utaratibu ukoje”alisema.

Naye Kaimu Meneja wa machinjio hiyo Florian Tillya alikiri kupandishwa kwa ushuru katika machinjio yake na kudai kuwa hali hiyo imetokana na mwekezaji ambaye anamiliki macnjio hiyo kampuni ya ya uwekezajiNICO kwa pamoja na Ranchi ya taifa ya NARCO.

Tillya alisema kuwa wafanyabiashara hao walipewa taarifa ya kupandishiwa bei ya ushuru tangu tarehe 8 Novemba mwaka huu machinjio hiyo ilipobinafsishwa na kuwa ushuru huo ulitakiwa kulipwa tangu kuanzishwa kwa machinjio hiyo mwaka 2003 lakini serikali ilikataa na ilikuwa ikitoa ruzuku y ash 9000 na fedha zilizoba walikuwa wakilipia wafanyabiashara hao.

Alisema kuwa kupanda kwa ushuru huo kunasababishwa na gharama za uendeshaji wa machinio kupanda ambapo alisema kuwa bei ya mafuta, na mishahara ya wafanyakazi viko juu kwa hiyo mwekezaji ameamua kupandisha ushuru kuanzia Desemba moja.

Ends………

4 comments:

Rama Msangi said...

kwahiyo krismass safari hii mmekula nini? Lakini Dodoma hamna shida bwana. Si mnakumbukia na kudumisha mila tu kwa kukandamiza lilende na ndigwa, siku zinapita na mambo yanaenda. Unajua itakuwaje siku makahaba pale Ohio watakapogoma? Unajua itakuwaje wale wajasiriamali wanaojazana Dodoma nyakati za Bunge, watakapogoma nao kuwepo mjini hapo nyakati hizo wazee wakiwa mjengoni?

John Mwaipopo said...

Kumbe bado upo? Vema sana.
Pengine sasa ni wakati wa watu kurejea bustanini kuchuma kisamvu na na matembele. Kwanza kufululiza nyama sio kuzuri kiafya. Shida ni mazoea. Poleni.

nyahbingi worrior. said...

samahani fungua kurasa ya kuchangia mawazo kuhusu jumuiya ya wanablogu tanzania.

http://blogutanzania.blogspot.com/

www.ringojr.wordpress.com

Anonymous said...

Duh Mtani kumbe mzuri hivyo! Basi dada Mungu alikusudia! Vipi mtoto wako ana miaka mingapi?