Tuesday, May 05, 2009

WENZETU HUKO TARIME wanadumisha mila kwa mtindo huu

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI LAWRANCE MASHA
AMA kweli ukistaajabu ya Mussa uyaona ya Firauni! wakati watu wanapinga mila na desturi zilizopitwa na wakati huko TARIME wenzetu wanadumisha tu!
hebu soma hii kwanza.

Katika mkoa wa Mara kuna mila ambayo imekuwa ikifanywa na wazee wa kimila ambao kutokana na kutekeleza mila hizo matukio ya mauaji yamekuwa yakisababishwa na mapigano ya koo mbalimbali.
Mila hiyo imesababisha hali ya ulinzi na usalama mkoa ni mara kutokuwa shwari na kutoridhisha kutokana na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya kiukoo, wizi wa mifugo, ujambazi wa kutumia silaha na biashara ya madawa ya kuelevya hususan kilimo cha Bangi.
Wazee wa Kimila Mkoani Mara ndiyo viongozi na waamrishaji wa mapigano ya koo yanayondelea, ambapo wazee hao hunufaika na mapigano hayo kwa kupata mgao wa mali zilizoporwa katika mapigano.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha anasema kuwa mila na desturi za baadhi ya makabila zinachochechea mapigano baina ya vijana wa koo moja na koo nyingine vitendo ambavyo vimekuwa vikiheshimika miongoni mwa jamii hizo kuwa ni vya kishujaa.
Waziri Masha anasema kuwa wazee wa kimila wamekuwa viongozi na waamrishaji wa mapiganmo hayo ambapo wamekuwa na maradaka makubwa katika Koo zao na hutoa adhabu kali kwa vijana wanaokwepa kushiriki mapigano.
Waziri Masha anasema kuwa kutokana na hilo, hadi sasa hali ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Mara si ya kuridhisha kwa kuwa kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya kiukoo, wizi wa mifugo, ujambazi wa kutumia silaha na biashara ya madawa ya kulevya hususan kilimo cha bangi.
Anasema kuwa matukio hayo yameenea katika wilaya za Tarime, Rorya na wilaya ya Musoma vijijini ambapo koo za hunyaga na Wamera na koo za Waanchari na Warenchoka na Wakira na Wanyabasi na Wairegi zimekuwa zikipigana mara kwa mara.
Masha anasema kuwa kilimo cha Bangi ambacho kimekuwa ni chanzo kikubwa cha uchumi kwa baadhi ya makabila katika mkoa wa Mara, pia kimekuwa ni chanzo cha mapigano hayo ambapo imekuwa ni kawaida kwa watu katika maeneo hayo kukodishwa na wakala kulima bangi na kulipwa fedha nyingi.
Anasema kuwa pale inapotokea kuwa mkulima wa Bangi aliyekodishwa hakufanikiwa kuvuna Bangi kutokana na Bangi hiyo kuharibika kutokana na ukame au kuharibiwa na vyombo vya dola, mkulima huyo hutakiwa kurudisha fedha alizopewa na wakala wake ambapo ili kupata fedha ya kurudisha, mkulima huiba ng’ombe za koo jirani na kuuza.
Waziri huyo anasema kutokana na mapigano hayo jumla ya watu 136 walifariki na zaidi ya 336 walijeruhiwa huku nyumba 2421 zikichomwa moto na kuacha zaidi ya kaya 756 zikiwa hazina mahali pa kuishi na vihenge 673 vya kuhifadhia mahindi kuchomwa moto katika kipindi cha kuanzia mwaka 2001 hadi machi mwaka huu.
Anazitaja hatua ambazo serikali imeshazichukua kuwa ni pamoja na kuifanya wilaya za Tarime na Rorya kuwa mkoa wa Kipolisi ili kukabiliana ipasavyo na matishio ya usalama, uhalifu na wahalifu.
Hatua nyingine ambayo Waziri Masha anaitaja kuwa ni ile ya serikali ya mkoa kupitia Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), kufanya kampeni mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi nyingine zikiwemo za dini, wanasiasa, wizara ya elimu na kushawishi wananchi kuachana na mapigano. Waziri Masha anasema kuwa mikutano ya ujirani mwema baina ya Vyombo vya dola vya Tanzania na Kenya inaendelea kufanyika ili kuimarisha mahusiano miongoni mwao, ambapo mapema mwezi.

HAYA AKINA MURA KAZI KWENU BWANA, IRA MUBADIRIKE ETI!

1 comment:

Ghati Chacha O'ghabhore said...

Samahani sana dada yangu lakini huu ni upumbavu na inanishangaza kwamba na wewe unaandika upumbavu huo huo bila ya kufanya utafiti. mimi ni mkurya wa kuzaliwa Tarime na sijawahi kusikia kuna mila ya watu kuuana. Matatizo ya Tarime na koo za kikurya ni makubwa na yanahusu influence za waKenya ambao wanafanya kila wanachoweza ili kuiba rasilimali kubwa ya wakurya ambayo ni ng'ombe. Serikali ilitakiwa kuungana na waKurya na kutatua tatizo hilo kwa kuzuia wizi wa ng'ombe ambao wanapelekwa Kenya. Tuna waziri mpumbavu ambaye anazungumza mambo ya kishenzi and then na wewe unaamua kuandika mambo hayohayo ya kishenzi humu ndani, eti wakurya wana mila za kuuana. Wacha upumbavu. Ni kweli Wakurya tunahasira kali, na hapa ninapoandika ninajiuma ulimi kwa hasiri....wacha ushenzi!