Wednesday, June 23, 2010

Et ni kweli kwamba kumkeketa Mtoto wa Kike kunamfanya asiwe Malaya?

HIVI ni Kweli eti kumkeketa mtoto wa kike ni kumfanya asiwe Malaya jamani? Ninauliza hivi nina maana, moja ya mila na tamaduni za wagogo hapo zamani ilikuwa ni kumkeketa motto wa kike ili kumfanya asiwe Malaya.

UNAOBA bwana, unajua kwa nini? Eti wabibi wale wa zamani wanasema kuwa ukimekeketa mtoto wa kike unampunguzia hamu ya kufanya mapenzi na hivyo anakuwa si Malaya!
Sasa sina uhakika kama ni kweli sana, naomba wadau mnisaidie katika hili tafadhali naombeni jamani, naomba mtoe maoni yenu halafu baadaye nitafunga mjadala kwa kuwa bado natafuta materials zaidi ya kuwafahamisha kuhusu mila hii ya mgogo!

Karibuni sana.

5 comments:

Anonymous said...

kumkeketa mtoto wa kike ni tendo la kikatili ambalo inaaminika na makabila mengi yanayo thamini mila hii kuwa inadaidia kupunguza umalaya.ndio kuna ukweli fulani kwakuwa sehemu inayo keketwa ni sehemu muhimu kwa mwanamke inayo amsha hisia za mapenzi hasa pale inapoguswaguswa.lakini ukeketaji na umalaya ni vitu viwili tofauti kwasababu umalaya ni tabia wala sio ugonjwa wakristo wanaamini ni pepo ambalo liikimwingia mtu anakua malaya haijalishi amekeketwa au la.kuna ushahidi mzuri kuwa ukeketaji hausaidii kupunguza umalaya kwa kuwa hao walio keketwa wamo baadhi ni malaya wa kutupwa.Ninacho jua ,mila ya ukeketaji iliandamana na mafunzo ya maadili mema kwa jamii hii ndio ilipunguza umalaya sio ukeketaji.wagogo katika kipindi hiki cha najando hufunza wahusika jinsi ya kuishi na jamii kwahiyo washiriki hutoka wameiva na kuhesabiwa ni watu wazima na hujitenga na mtu yeyote ambaye hajapitia hatua hata kama ni mkumbwa kupita wao huhesabiwa ni mtoto.mimi nelson chilongani

Martha Mtangoo said...

Ni kweli kaangu, umalaya ni tabia haihusiani na kukeketwa, lakini eti wanasema akikatwa kale kadude hamu ya kufanya ngono inapungua sana, hata huyo pepo anatoka, wewe unasemaje?

Anonymous said...

narudi tena kukuhabarisha wee kalumbu.kama nilivyochangia mara ya kwanza nilikubali kuwa ukeketaji ni ukatili ambao unampunguzia mwanamke hamu ya kufanya mapenzi ila haimalizi hamu ya kufanya mapenzi.ukizingatia kuwa sio kale kadude peke yake kanako tengeneza hamu au nyeke,kwahiyo ukeketaji ulilenga kupunguza nyege mshindo lakini ile ya kawaida inabaki palepale.nikasema kuwa ,mafunzo katika kambi za ukeketaji ndio yalisaidia wanawake wawe na maadili mema lakini sio kitendo cha ukeketaji.kwahiyo nashauri zile kambi zifufuliwe ila ukeketaji ukomeshwe.sio vema mtoto wa kike kuingia utu uzima bila mafunzo ya msingi ya maadili na elimu ya asili ya uzazi ambayo ina njia bora za kiasili za uzazi wa majira na mitindo ya asili kwenye sita kwa sita kiasi ambacho ukibahatika kumpata mke aliyepitia madarasa haya ya jadi hutasahau.Naungana na wataalamu waliotafiti na kutuhabarisha kuwa ukeketaji unaacha kovu ambalo linaleta athari kubwa kwa mwanamke hasa wakati wa kujifungua.Tukubali Mungu kaumba kila kitu na kazi yake sasa ufundi wa nini kwenye mwili wa mutu. sina mengi mimi chilongani

Martha Mtangoo said...

sawa kaka umeeleweka, hapo nimekuelewa sanasana, kuna baadhi ya makabila bado wanaendeleza mila hizi lakini yapo pia makabila yanafanya kuwafunda watoto wa kike pale wanapovunja ungo bila kuwakeketa ni vizuri basi makabila mengine yakaiga huu utamaduni. lakini hofu ya kaka kuwa asipofundwa atashindwa mambo fulanifulani katika ndoa, siku hizi mambo poa kakaangu, kuna kitchen party kabla ya kuolewa na ambayo inatoa mafundisho mazuri sana kabla ya kuolewa na akatimiza majukumu yake kama kawaida bila shida. asante sana kakaangu nitatoa hitimisho lango hapo juu kila mtu aone.

Anonymous said...

Ukeketaji haupunguzi umalaya bali unaharibu shape tu ya sehemu nyeti ya mwanamke. Ninayo mifano mingi ya watu waliokeketwa na kuwa bado malaya kibaya zaidi wengine ni wake za watu. Ingekuwa kukeketwa ni kupunguza umalaya hawa wake za watu pamoja na kuwa wamekeketwa na wameolewa mbona bado malaya? Kwa hiyo umalaya ni tabia ya mtu mwenyewe wenzetu wanaita "trait"