Monday, July 18, 2005

Wizara Nyeti ambayo Waheshimiwa Wabunge hawaifahamu!!!


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

WIZARA ya Maliasili na Utalii ni Wizara NYETI ambayo watu wengine bado hawajatambua Unyeti wa Wizara hii, inaniuma sana.

Nafikiri kila mtu anajua ni kwa nini hilo linaniuma saaana, Utamaduni wetu watanzania ni pamoja na mali ya asili ambayo ni Misitu na hifadhi za wanyamapori.

Naumia sana kwa maana Utalii ni pamoja na Wanyamapori, Milima, Maziwa na Mito ambayo ipo hapa Tanzania.

Sasa hebu fikiria kinachonisikitisha zaidi ya yote ni kwamba hata Waheshimiwa Wabunge wenyewe wa Bunge la Jmhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (TANZANIA), hawajui kabisa kuwa Wizara hii ni Nyeti.

Utajuaje kama hawajui kuwa Wizara Nyeti sio Nyeti, ni hivi kwanza Wizara hii haina msaidizi kabisa, Mwanamama
ZAKIA HAMDANI MEGHJI anafanya kazi Mwenyewe kama Waziri wa Malisili na Utalii.

Ni kwamba wabunge walishindwa kushinikiza kuwa Wizara hiyo Nyeti iwe na Msaidizi yaani hapa naamnisha kuwa Wizara hiyo haina naibu waziri.

Mama huyu pamoja na kutokuwa na Naibu Waziri kama ilivyo wizara nyingi tu ambazo zingine zina manaibu Waziri watatu kama ilivyo Wizara ya Fedha anafanya vizur sana.

Angalia Watalii wameongezeka kutoka 295,312 mwaka 1995 hadi kufikia 582,807 mwaka 2004, hii ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 10 kwa mwaka.

Hali kadhalika mapato yatokanayo na utalii yameongezeka toka dola za kimarekani milioni 259.4 mwaka 1995 hadi Dola milioni 746.0 mwaka 2004 mabpo mpaka mwaka huo Sekta hiyo ilikuwa imetoa ajira kwa watu wapatao 199,000.

Sasa kwa nini mama huyu ambaye anautangaza utamaduni wa Mtanzania nje ya Tanzania asiwe na Msaidizi? Haya nikisema utasikia ooh wanawake bwana wanataka dezo hatutaki dezo na kazi tuweza sana, Hongera sana Mama Meghji kwa kazi nzuri.

Lakini ni vyema Serikali ya awamu ya nne ikazingatia ushauri huu kuipatia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuwa hii ni Wizara Nyeti kama zilivyo wizara nyingine ikiwezakana atoke Wizara ya Fedha azibe nafasi hiyo.

Angalia utalii wa Tanzania hapa uvayotangazwa bila upendeleo hiyo ikiwa ni kazi ya Mwanamama na mwaka huu anagombea hataki viti maalum tena!!!!!!!

3 comments:

Indya Nkya said...

Nadhani ungetoa pendekezo kwamba cheo cha unaibu waziri kifutwe kama Wizara kama hiyo inakuwa haina Naibu Waziri na kazi zinaendelea kwa nini wizara nyingine ndogondogo ambazo zinatakiwa ziwe idara tuu ziwe na naibu waziri? Hebu fanya utafiti naibu waziri ana kazi gani? Angalia pia wizara ya Ulinzi na JKT haina Naibu waziri. Je inafanya vibaya kuliko wizara zenye naibu mawaziri? Huo ungekuwa uchambuzi wa kina sana

Anonymous said...

MAMA U R VERY CREATIVE YOTE TISA KUMI HUYO SHOGA ALIYEUKWAA KANIMALIZA NGUVU ZOTE ZA KIKE!KHA!KWA KWELI PICHA HIYO ITAKUWA FUNDISHO KWA YEYOTE MWENYE MACHO ATAKAE FUNGEA:SASA BASI IWE KWELI MAJUTO KUTOKA ROHONI NA TUBADILI MWELEKEO NA MTINDO WETU WA MAISHA KWANI DUNIA INAANGAMIA MAMA!LOH TUANZE BASI SISI WAANDISHI HUSUSANI MABINTI KWANI TUNAKUA TUNAACHIA NA KUNYWA CHAI ZA MOTO KAVUKAVU!PIA TUMRUDIE MUNGU MANAKE HIVI VYAWEZA KUWA VISHAWISHI KUTOKA KWA IBILISI,ILA TUSIJE TUKAMSINGIZIA SHEITWAN ILA TUBADILI TABIA LA SIVYO TUTAANGAMIA JAMANI,UKIMWI UNAUA CHAI NAZO TWAZITAKAi MH

KEEP IT UP LADY!

Anonymous said...

Kwa unyeti huo huo hiyo wizara asingepewa huyu mama. Mali ya asili na utalii unakwenda kumpa mtu mwenye asili ya Kihindi. Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana!

Zakia Meghji hawezi kukasirika akiuona ujumbe huu kwa sababu anajua kabisa hata huko kwao India kuna suala la uchaguzi/ubaguzi wa nani ashike nini kufuatana na mfumo wao cast/kupangana madaraja ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa.
Bibi Sonia Gandhi mwenye asili ya Kitaliano alipingwa na Wahindu wenye msimamo thabiti ili aachia nafasi ya uwaziri mkuu kwa sababu ya asili yake na alifanya hivyo.
Siku Wahindi wakianza kuoa na kuolewa Watanzania asili, kuishi Sinza, Mwananyamala, Magomeni, Manzese nk. Halafu wakaanza kuwa watumishi wa serikali wa nngazi zote siyo uongozi tu tena uongozi wenyewe ni ubunge na uwaziri pekee yake, wawe makondakta wa daladala, walimu, wauguzi, makarani, madereva nk wa taasisi za serikali hapo ndipo nitaungana nao vinginevyo ni upumbavu tu kujifanya kuwa nao karibu!