Sunday, September 11, 2005

Mzee wa Miaka 85 kuhutubia Umoja wa Mataifa, Yuko Darasa la Pili

AMA kweli Elimu haina Mwisho, kwa hili unaweza ukaamini kwamba ni kweli sasa hii ni karne ya Sayansi na Tekonoljia na Si zama za mawe za Kale.
Enzi za ujana wetu miaka ya 47 hakukuwa na kitu kama hiki na wala utamaduni kama huu haukuwepo wa kikongwe kusoma ete anaanza darasa la kwanza akiwa na miaka 84 haya ni maajabu! tena ya Musa.
sasa hebu hapa uhondo kamili hapa

3 comments:

Reggy's said...

sikuona kiunganishi cha habari hii, ukifungua kinafunguka kitu kingine.

Rama Msangi said...

hiyo ni ishara ya mwamko wa hali ya juu wa waafrika katika kujikomboa na madhila mbalimbali yanayowazunguka, maana mkombozi wao pekee ni elimu. Tatizo ni kuwa je elimu hiyo inaweza kweli kuwakomboa kutoka makucha ya walafi wa kizungu ilhali mitaala yenyewe ya elimu inaigwa kwa hao hao tunaodai wanatukandamiza??

Ndesanjo Macha said...

Habari hii imenimaliza nguvu ila nimefuatilia kiungo niipate zaidi bila mafanikio. Kiungo kiko wapi?