Monday, April 03, 2006

Amini! Gari ya hakimu iliyoibwa yapatikana!

Gari ya hakimu iliyoibiwaimepatikana eneo la Yombo Buza wilayani Temeke. Gari hilo limepatikana likiwa limeng'olewa Vipuri mbalimbali ikiwemo vyenye thamani ya sh. milioni 1.1.

Hakimu safari alisema kutokana na gari hilo kutokuwa na mafuta ya kutosha ndio sababu iliyowafanya wezi hao kuliacha gari hilo baada ya kuishiwa mafuta. Gari hilo linashikiliwa katika kituo cha polisi Chang'ombe na Polisi bado wanaendelea kuwasaka walioiba gari hilo!!!!!!!!! haya mnasemaje?????

4 comments:

MK said...

Dada Martha Beatrice Mtangoo kuhusu swali lako nimeshakujibu.

Naomba bonyeza hapa uende kusoma majibu yake.

Nashukuru,
©2006 MK

Jeff Msangi said...

Hii ni kama lile alitakalo Mwandani la kipindupindu kubisha hodi ikulu siku moja.Nadhani kama jeshi la polisi halijalewa sifa za vyombo vya habari bado litaamka na kujua kwamba kazi bado wanayo.

John Mwaipopo said...

Hii balaa. watapata akili litakapoibiwa la Kamanda Mwema au la JK mwenyewe

Rashid Mkwinda said...

Hili la Hakimu kuibiwa gari ni la aina yake hivi sijui huyo mwizi akipatikana na akafikishwe mbele ya hakimu aliyeibiwa ili atoe hukumu ya kesdi hiyo sijui itakuwaje?mi nadhani itakuwa kama kesi ya Panya kumpelekea Paka ahukumu