Monday, July 11, 2005

Inapofikia hatua Mtoto Anazaa Mtoto Mwenzie!! What has become of mankind?

Ama kweli sasa tulipofikia ni Karibu na Mwisho, Hivi Yesu atarudi lini? kila mtua ana majibu yake wengine wanasema alisharudi wengine wanasema arudi kufanya nini yote Kheri lakini na tumuombe sana atausaidie kuelewa.

Hii ni picha ya Mtoto mwenye umri wa miaka 10 tu! wa Wilaya ya Kericho Nchini Kenya, kila mtu atauliza sasa kma wa Kericho Nchini Kenya si tufanyaje, Sikiliza ni Mtoto wa miaka 10m ambaye miezi michache iliyopita alikuwa akicheza na wenzie michezo mbalimbali akirudi Nyumbani anaogeshwa lakini sasa amekuwa mama wa Mtoto Jamani tunaenda wapi?!

Kinachoniuma zaidi ni kwamba Baba Mtu mzima ana akili zake ameamua kumfanyia hivi huyu mtoto mdogo ambaye ni sawa na mwanaye wa kumzaa jamani inatia uchungu sana sijui ni wapi tunaelekea Mungu tusaidie kuelewa nini Tunatenda.

Inauma sana, inakatisha tamaa, hebu fikiria mtoto mdogo namna hii anamnyonyesha mtoto mwenzie amezaa anaweza kulea? anaweza kujua iwapo leo mwanangu anaumwa sasa nimpeleke Hospitali? wewe Baba Jitu Zima umemtafutia matatizo ambayo yanamfanya mtoto anaingia katika kitabu cha historia wewe umepumzika.

Ukimuuliza alikuwa anatafuta nini kwa mtoto mdogo tena bado ananuka Shombo kali madai yake mtoto mdogo hana Ukimwi, hatakuwa na ukimwi wakati mizee mizima inataka watoto wadogo?

Na Walaaniwe wote wenye tabia mbaya inayomsababishia mtoto mdogo matatizo katika Siku zote za Maisha yake.
Unakaribishwa kuchangia Bila Jabza wala Upendeleao wa Kijinsia Karibu.

What has become of mankind?

This is a picture of a 10 year old lovely school girl,from the Kericho District in Kenya.
What makes her sospecial? With her whole life ahead of her, a wonderful futureto strive for an education and to move into her teenyears and have fun playing with her fellow girls,children of her own age, she is not playing withdolls.
She is handling the real thing. She has becomea Mother.
Definitely there is a Man somewhere who is to blame!What has become of mankind?People have no fear of the Creator, the Most Merciful,the most Benevolent.
Are we coming to the end?

3 comments:

mwandani said...

Walaaniwe makafiri!

Ndesanjo Macha said...

Huu ndio unaitwa umaaluni wahedi! Wapi tunakwenda?

Anonymous said...

Loo, nilifikiri huyu mtoto wazazi wake wamekufa na ukimwi na yeye anatunza mdogo wake. Mhh, tumekuwa kama Philippines vile maana huko nasikia ile mizee kutoka Europe ikisikia kibinti kina miaka 10 basi wanasema "sikitaki hiki kizee". Ama kweli dunia yetu sasa ni KIJIJI - YAMESHAFIKA.