Tuesday, August 02, 2005

Si Ulitaka Chai! Iweje ulalamike Unaungua?

Baada

Haya Jamani tukiambiwa tuache kunywa Chai kavu tunang'ang'ania Tu na Matokeo yake ndo haya Tunaungua, Kunywa chai na Vitafunio hata ikiwa ya Moto Kiasi gani huwezi Kuungua kama ilivyomuunguza marehemu Mrembo Huyo ambaye alikuwa akisoma Chuo Kikuu cha MOI huko Nchini Kenya.

Alipojijua kama ameambukizwa Virusi ya Ukimwi akaahidi Kulipiza Kisasi kwa yeyote ambaye atakatiza Machoni Mwake na alifanikiwa kuambukiza Jumla ya Wanaume 124 nchini humo ambao waliopona ni 6 kwa kuwa walimua kunywa chai na Vitafunio.

Kabla alikuwa Mrembo sana kama anvyoonekana katika Picha ya Chini
Nawaombeni sana Radhi Wapenzi wasomaji wa Blog yangu, kwa kuchapisha Picha ya Kutisha namna hii hii inasababishwa na Mimi kuguswa sana na Tukio hili.
Kunyweni Chai na Vitafunio Jamani la Sivyo Tutaungua!

6 comments:

ARUPA said...

Du! mama unanitisha sana kwa hilo onyo lako lakini sometimes chai kavu ni tamu sana kuliko chai yenye vitafunio kwani ukiitumia yenye vitafunio unakuwa ume-dirute utamu asili na inakuwa sio Concentrated, utamu woote unaisha kabisa lakini inabidi tujifunze kunywa chai na vitafunio kwa sababu tunalazimika na tusipofanya hivyo chamoto tunakipata, lakini naomba nikuulize kati ya chai kavu na yenye vitafunio ipi tamu?

mwandani said...

ahsante kwa 'shock therapy'Tutahadhari lakini, si masihara haya.

Egidio Ndabagoye said...

Si unawafahamu wanaume famili wanasema "ulinunua kwa goto sasa mbona unasema unaungua?... si ulimuona kifaa sasa ushauvagaaa"

Reggy's said...

Nakubali ujumbe, sikubali idadi ya walipitia kwa dada huyu. Kwa nini? Nani aliwahesabu? Alijuaje kuwa watu hao walikuwa na ukimwi kabla ya kukutana na huyu dada? Alijuaje kuwa kila aliyelala naye (chai Kavu) aliambukizwa? na maswali mengine kadhaa. haya ndiyo kazi ya Dereva Taxi Adam wa Dodoma, anayedaiwa kutembea na watu 400. (Ingetokea akalala na wawili kila siku, ingemchukua miezi sita) kuwamaliza. Alikuwa na pesa kiasi gani cha 'kuwaweza wote hao?

Anonymous said...

ndugu yetu martha we umepima au