HAKI ya Mungu yaani Chama cha Tanzania LabourTLP kina mbwembwe kweli kweli! Zile za CCM ni cha mtoto wanawake sasa sawa na wanaume yaani wee acha tu.
ni kwamba hivi karibuni chama hicho kimemsimamisha mgombea mwenza wa urais mwanamke ambaye atakuwa akigombea nafasi hiyo na Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Augustino Lyatonga Mrema mwezi oktioba mwaka huu.
basi bwana wamemsimamisha mwanake awe mgombea mwenza wa nafasi hiyo kwa madai ya usawa unazingatiwa katika chama hicho ambacho hivi karibuni tuu kimepata ruzuku baada ya msajili wa vyama vya siasa nchini Bw. Tendwa kutangaza kuwa anakitambua chama hicho.
lakini sasa huyo mgombea mwenza anavigezo vya kuwania nafasi hiyo?
kwa kuzingatia yafuatayo wenyewe mtasema kama vigezo anavyo ama laa!
* Je Ikulu ni Maabara ya kufanyia majaribio ya uongozi?
* Ikulu ni mahali patakatifu amejitakasa?
*kazi ya urais si ya kubeba zege Bongo yake inachemka?
*utamu wa komamamnga ni komamamnga lililokomaa, amekomaa?
Angalizo: USHUZI HAUZIMI MOTO! Mnakaribishwa kuchangia maoni yenu bila woga wala Jabza na kutopendelea kwa aina yoyote, karibuni sana.
1 comment:
Kuna siasa Tanzania au kuna SIHASA??, ukilijua hili ndugu yangu naamini hakuna luitakalokutatizo kabisa, sio akina mzee wa Kiraracha na wenzake katika genge lao bali na wengine wooooooote.
Post a Comment