Monday, May 09, 2005

Wengine walishehekea hivi Siku ya mama!

Tarehe 8 May kila mwaka duniani kote husherehekea siku ya mama Yaani Mothers Day!

hapa kwetu Tanzania watanzania nao pia walisherehekea siku hii kwa furaha kubwa ikizingatiwa siku hii iliangukia katika siku ya Jumapili ambayo ni siku ya mapumziko ya mwisho wa wiki.

wengine walisherehekea siku hii kwa kuwashukuru mama zao kuwaweka hapa duniani kwa kuwazaa, kuwalea na kuwapatia kila kilicho mahitaji yao na kuwafikisha hapo walipo sasa.

wengine waliwapatia mama zao zawadi mbalimbali ikiwemo kadi, maua na zawadi nyinginezo nyingi kwa ajili ya kuonyesha upendo wao halisi kwa mama.

lakini kwa upande wa wa wafanyabiashara hali kwao ilikuwa tofauti na wengine kwa kuwa wafanyabaishara wao walikuwa wakifanya biashara kwa kuuza kadi za siku ya mama na maua kwa ajili ya siku hiyo.

mwanzilishi wa siku hiyo Bibi. Anne amekilaani kitendo hicho cha kufanya biashara kwa kusema kuwa kuwa lengo la siku hiyo halikuwa kufanya baishara kama wanavyofanya sasa watu wengi hapa duniani.

anasema kuwa lengo la kauzishwa kwa siku hiyo ni kuwapongeza akina mama ambo walikuwa wakiwapokea waume zao ambao walikuwa wakirejea kutoka vitani ambao kabla ya kuondoka waliawaacha akina mama hao wengine ama wakiwa na watoto wadogo ama mimba ambazo akina mama hao pamoja na kupata shida zote za upweke waliweza kuwalea watoto wao na kaundaa mapokezi kwa ajili ya kuwapokea waume zao ambao walikuwa wakitoka vitani.

upendo huu waliouonyesha akina mama hawa ulisababisha kuanzishwa kwa siku hii muhimu sana na siyo kwa ajili ya kufanya baishara kama ilivyo sasa. HONGERENI AKINA MAMA!

2 comments:

Indya Nkya said...

Lakini watanzania wanaiwekaje hii siku kufuatana na mazingira yao? Kama nikimnunulia mama yangu aliyeko kijijini kadi ambayo imeandikwa kwa kiingereza sijuhi kama kwanza anathamini hiyo kadi achilia mbali kuelewa kingereza. Sikukuu hizi ni lazima zizingatie tamaduni zetu si kuzichukua kama zilivyo

Ndesanjo Macha said...

kwanza mimi ukininunulia kadi au zawadi kwenye siku ambayo imetengwa na watu ambao wala huwafahamu nitakurudisha na hiyo zawadi yako. Huko ni kuwa kama mashine. Eti unipe zawadi mwezi wa pili mwaka huu na usubiri hadi mwezi wa pili mwakani. Huo ni utumwa. Nipe zawadi unapojisikia kunipa zawadi sio kwa kuwa kuna kitu mnakiita Valentino ndio unajifanya kuwa nawe una utamaduni wa kununua maua na kadi. Maua huyapendi mwaka mzima, unayakanyanga, huyaoni, huyamwagii maji lakini unajifanya kuninunulia! Kwanza unanipa kadi ya nini? Nipe parachichi!