Saturday, May 28, 2005

WANAWAKE BWANA...........! YAANI AKULETEA VIRUSI NA UNAVIPOKEA KWA MIKONO MIWILI

KAMA mkeo au mpenzi wako anatoka nje ya ndoa na unajua kabisa yaani una uhakika utafanya nini?

Jibu la swali hili kwa wanaume wengi litakuwa ni lenye kuashiria maumivu kwa upande wa pili.

kwa vipi sasa?

jibu linaweza kuwa nitamwacha hapahapo au nitamwua ama tutakufa wote mimi na yeye, hayo yanweza kuwa majibu toka kwa mwanaume ambaye amefahamu hilo.ni amjibu ambayo ni ya kishujaa eh!

iwapo mwanamke angeulizwa swali hili unadhani angelijibu vipi?

bila shaka angelijibuhivi; 'nitaondoka au nitamkomesha huyo hawara yake ama shauri yake mwenyewe mimi si nitaendelea na maisha yangu' haya ni majibu muafa ya kinyonge eh!

kwa kawaida wanaume hawako tayari kusamehe kosa la kutoka nje linapofanywa na wake au wapenzi wao, ni wachache sana wanaoweza kusamehe.

sisemi kwamba hakuna wanawake ambao nao huchukulia kutoka nje kwa waume zao kama jambo lisilo sameheka, kiwango cha wanawake hao ni kidogo sana ikilinganishwa na kile cha wanaume ambao hawako tayari kusamehe uzinzi wa wake zao ama wapenzi wao.

wanaume saba kati ya kila kumi hutoka nje, tafiti zinaonyesha kuwa wanawake karibu watano katika kila kumi wanajua kuwa wanaume wao htoka nje lakini huwa hawana la kufanya, wameamua basi!

alkini wanawake wanane katika kila kumi wanajua kwamba waume zao wanatoka nje na wanachukua hatua za kupambana na hali hiyo wakiwa ndani ya ndoa zao, wakati ni mwanamke mmoja katika kila wanawake kumi ndiye huondoka kwenye ndoa ya aina hiyo. hii siyo taarifa nzuri kwa akina mama.

KUKUBALI kuishi kwenye ndoa ambapo una uhakika kabisa kwamba mwenzako anakwenda nje kutafuta kifo huku akikufuja kwa njia moja ama nyingine ni kujishusha sana, kuna wale wanaosema shauri lake kwa sababu wameshakubali kwamba wao ni watumwa wa hao wanaume bila kufikiria.

hivyo wana haki ya kupangiwa nao hata siku ya kifo, hapa wanawake na wasichana ni lazima tuwe macho na tuamke sasa tukiendelea kuishi maisha ya namna hii matokeo yake tutakuwa tunasubiria kuletewa virusi vya UKIMWI na tunavipokea kwa mikono miwili na badae tunakufa kwa ugonjwa wa Ukimwi kwa madai kuwa Mungu katutenganisha.

2 comments:

mwandani said...

Hii habari ya uzinzi, kama maovu ya rushwa katika jamii yetu yanachukuliwa kama kijisifa.Kwamba fulani kapata ulaji, Kwamba fulani mtu wa watoto nk. Wala mtu hapepesi macho kwa mshangao kwanini mtu anaenda kutembea nje bila mpango. Tena mama wa nyumba ndogo hana wasi kama anakatiwa kitu kidogo ilhali anajua mshefa kaoa.
Mie nawashauri akina dada msimame kidete.Msimamo mpaka muone mwisho wake. hakuna nini wala nini. Kwani ukimwi unatuondoa kikweli.
Na sie madume tujirudishie maadili, japo tushapotoka kwa sana, lakini tunaweza. Najua ni vigumu kwa wapenda zinaa kuwacha,Hatuwezi kuwa wanaume kweli ikiwa tuna udhaifu tusioweza kuukabili. Huo ni umajinuni.

Mija Shija Sayi said...

Habari kabambe!! inahitaji majadiliano ya kina, imenipa fikra nyingi, nikaanza kulinganisha kama tatizo hili lingempata mwanamke wa kijiji ambaye hakwenda shule angelitatuaje kulinganisha na wa mjini tena aliyesoma, na je maamuzi yao yangeisaidiaje jamii katika kumtathmini mwanamke??

Hebu mtani nisaidie hapa....kama ni wewe unagundua mumeo ana mahusiano nje ya ndoa yenu ungeamuaje?? na unadhani uamuzi wako utaisaidiaje jamii kujirekebisha?