Tuesday, May 17, 2005

Itafika wakati hata Jogoo watawika Kwa Lugha ya Kiingereza!

Tangu enzi za mababu zetu watanzania tumekuwa tukijitahidi kuenzi utamaduni wetu na hasa baada ya kupata uhuru wetu mwaka 1961 chini ya Mwl J. K. Nyerere wee acha tu.

licha kuwepo kwa juhudi za kuuenzi utamaduni wetu wa kitanzania pia kupitia lugha yetu ya taifa ya kiswahili tumekuwa tukiitumia sana katika kuuenzi utamaduni huu kuanzia katika shule za awali hadi vyuo vikuu.

kutokana na watanzania wengi kujitahidi kuendeleza zoiezi zima la kuuenzi utamaduni wao kumekuwapo na vikwazo kibao ambavyo vimekuwa vikiwafanya watanzania hawa kushindwa kuendelea katika suala la kuuenzi utamaduni kutokana na baadhi ya viongozi wao kukazia kutumika kwa lugha ya kiingereza.

kutokana na watanzania kukaririshwa kuwa kiingereza ni lugha ya kimataifa na kutokana na tanzania kufikiria tena kuingia katika shrikisho la jumuiya ya nchi za afrika mashariki hapa watanzania wamekuwa wakichanganyikiwa sana.

kinachowachanganya ni kuhusiana na hiyo lugha wanayoambiwa kuwa ni ya kiamtaifa kama huijui huwezi hata kufanya biashara ya kuku nje ya nchi, kikubwa zaidi kinachowachanganya watanzania wanaoishi kule mvumi kuhusiana na wao kufanya biashara nje ya nchi wakati hata 'kiswakigo' (kiswahili Kigogo) chenyewe kimepita kushoto.

lakini kinachowachanganya zaidi ni suala la kuwafundisha mbuzi wao wanaotegemea kwenda kuwauza nje ya tanzania jinsi ya kulia kiingereza au jinsi ya kuwafunda kuku wao jinsi ya kuwika kiingereza wanapokuwa katika masoko nje ya Tanzania.
Itakuwa ngumu sana kufamnikiwa katika suala la kuuenzi utamaduni wa mtanzania kupitia katika lugha ya taifa ya kiswahili huku viongozi wakisisitiza kuwa kiingereza ni lugha ya kiamataifa, umefika wakati ambapo mataifa mengine waambiwe kuwa kiswahili ni lugha ya kiamataifa.

ili nao waanze kuwafundisha kuku wao kuwika kokoriiiko yaani kwa kuwika katika lugha ya kiswahili au waanze kuwafundisha mbuzi wao kulia kwa lugha ya kiswahili Meeemeeeee! ili tufikikie malrngo ya kuuenzi utamaduni kama wao walifanikiwa.

2 comments:

Indya Nkya said...

Uwakumbushe kwamba wachina wanaotawala dunia kwa bidhaa zao wao kiingereza chao ni babaishi kabisa. Huwezi kufanya ugunduzi kwa lugha unayoiba unababaisha huwezi hata kuandika ukaeleweka. Wajerumani, wafaransa na wengine wote huenzi lugha zao

Rama Msangi said...

'Chidumu Chitendekunu', yaani itakuwa kaaazi kweli kweli dada maana mhh, sijui itakuwa vipi kwasababu sisi wenyewe tumeshindwa kukijua hicho 'Chitzungu'tunavunjia vunjia tu alhamdulilah, sasa hawa mbuzi wetu sijui inakuwa vipi hapo.